Enigmatic_
Member
- May 12, 2023
- 16
- 13
Kama ilivyo kawaida kwa vyuo vingi vya elimu ya juu kutoa ufadhili kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu, chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kina utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa ngazi ya shahada za awali na shahada za uzamili.
Katika mwaka wa masomo 2022/2023, dirisha la maombi ya ufadhili lilifunguliwa tarehe 20/09/2022 na kufungwa tarehe 15/10/2022, huku majibu (kwa washindi) yakitarajiwa kutolewa wiki nne baada ya kufungwa kwa dirisha la maombi. Mara nyingi, kwa utaratibu uliopo, washindi hutangazwa hadharani kupitia tovuti ya chuo. Cha ajabu na cha kusikitisha, leo ni karibu miezi sita bado majibu hayajatolewa.
Je! Kuna nini nyuma ya pazia? Hakuna uwezekano kwamba kuna 'wachache' waliopewa ushindi kimyakimya? Inafikirisha na kusikitisha hasa kwa taasisi kubwa kama UDSM kufanya kosa kama hili!