Udsm vs udom

Udsm vs udom

Nancheto

Member
Joined
Mar 4, 2011
Posts
25
Reaction score
4
Nimekuwa nikifuatillia mijadala kadhaa kuhusiana na ubora wa elimu ktk vyuo vikuu vyetu hapa TZ na wengi wakitoleana maneno
yenye kadhia na wengi wao wanapigia upatu vyuo vya UDOM na UDSM.Vijana wanagombea fito ilhali nyumba ni moja!Mimi ninafikiri watz
wangejadili vile vyuo ambavyo hata udahili wake haukidhi vigezo vya TCU.vyuo hivyo TCU inavifahamu na bado inavifumbia macho.
kwa mfano kuna vyuo vikuu vinadahili wanafunzi wenye div 4 hadi pts 29!Je tunategemea nini?Nadhani tuendelee kuvipa moyo vyuo vikuu
vyenye kuonesha azma ya kuliendeleza taifa letu na si kuviponda.hivi mulitaka hadi leo tuwe na UDSM pekee?Je mulitegemea UDSM ingetoa promo ili wanafunzi wakasome hapo?tazama sasa wanafanya hivyo,haya ni maendeleo makubwa.waswahili wanasema mkeo akiwa na gubu
muolee mke wa pili.Tukumbuke Roma haikujengwa siku moja.Naomba nimalizie kwa kusema hivi tutoe michango itakayoboresha elimu yetu
ya juu kwa mustakabali wa nchi yetu.

SCHOOLING IS USELESS BECAUSE SCHOOLS ARE MAKING PEOPLE MORE STUPID AS HOSPITALS ARE MAKING PEOPLE MORE SICK:IVAN ILLICH 1926-2002.
 
Thanks mkuu. Tujitahidi kuangalia mambo ambayo yatatutoa kwenye umaskini tulionao! Udsm ni babaake Udom,so as times goes on itakuwa like father like son.
 
hizi mada za udsm vs udom zimekua nyingi sana na tumezichoka,Mod naomba thread hii iondolewe
 
competency ya graduant wa chuo inajengwa kwa juhudi zake na elimu ya juu inakupa mwanga wa kuwa mdadisi, mhojaji, mtafutaji, mfuatiliaji, mzalendo, mkemeaji penye kosa, mshauri nk. na haya yote ni zao la elimu+attitude. so, ishu ya vyuo si hoja na pia tuwe makini na baadhi ya posts, kuna form 1-4 wanaingia humu na kupost chochote tu, tukumbuke our motto of JF, the home of great thinkers. lets not deviate from from the point.
ahsante
 
Hii thread imenyooka alafu imepinda,unavikandia vyuo vinavyodahiri failures alafu unaikandia Udsm,how?mie nadhani leo ingetosha ukaongelea udhaifu wa vyuo vikuu vinavyodahiri failures alafu siku nyingine ukaongelea mchango wa uwepo wa vyuo vikuu vingi nchini kuliko kuwa na double role per time...obligado!
 
Back
Top Bottom