UDSM yashuka kwenye list ya 'Top African universities'

Hahah..
Sikushangai.. jina lako linakusadifu wewe ni mtu wa aina gani!
Kwa Tanzania sioni chuo chochote chenye quality ya UDSM

We are talking about its rank among other quality universities in AFRICA, sio TZ. hata miongoni mwa majuha huwapo mwenye nafuu kuliko wengine

Kwa hali kama ile mlimani lazma tu kiwango cha elimu kishuke, kwa sasa pale ni siasa mbele, elimu baadae na ndo maana migomo haiishi pale,wanafunzi wa pale full stress!!!!!!!

Mkuu naomba nikubaliane na wewe kwamba migomo inachangia kushuka kwa elimu ila naomba nipingane na wewe kwamba UDSM migomo haiishi nadhani siku hizi afaddhali ukilinganisha na kinachotokea UDOM. Kwa hiyo ukweli unabaki kuwa huenda ndio maana UDOM haimo kwenye 100 bora!

Mbona vyuo vikuu vingine kama Tumaini, Mzumbe, SUA n.k. sivioni kwenye hiyo ranking?

Mbona ulichosoma wewe (Tumaini University) hakionekani kwenye hiyo list/ ranking?

Very bad indeed!! Mbona univesite nyingine hazija-appear kama vile Muhimbili University of Health and Allied Sciences, UDOM, KCMC, Kairuki, Bugando, etc?? Hazijulikani nini??

Tatizo lako ni hicho chuo cha saint kayumba ulichosoma 1st degree kwa kubebwabebwa ukitegemea mtelemko hapa udsm.pole sana kaka udsm mziki mnene hakuna kubebana kama huko kwenu. Usitake watu waamini ukilaza wako.je chuo ulichosoma nicha ngapi africa na duniani?mbona vyuo vitatu nigeria vimeshuka kwa nafasi zaidi ya kumi hamjasema.tatizo lenu kushindwa kuja udsm kwa ukilaza wenu kunawasumbua na hataki kuamini kuwa hiki ndo chuo mama cha taifa kwa kila kitu.najua ulitegemea kupata gpa ya 5 kama huko saint kayumba ndo maana unawponda maprof baada ya kunusurika kufeli.pole sana kaka udsm haifananishwi na chuo chocote tanzania.''we are the cream of the country'

Mbona kwenye hiyo list sikuiona Muhimbili University, chuo cha madaktari bingwa???????? bongo bwana eti madaktari bingwa... lol
Una hasira na muhimbili. NI KWELI HUWEZI KULINGANISHA MUHIMBILI NA UDSM, MUHAS WAKO JUU SANA KWENYE PRACTICAL ISSUES. KINGINE NI SUA, HUWEZI KULINGANISHA ELIMU WANAYOPATA WATU WA SUA & MUHAS NA WADESAJI WA UDSM. UDSM NI JINA TUU BUT PRACTICALLY IT IS A CRAP.HAKUNA KITU PALE NI SIASA TUU, UKIMWI, MISONGAMANO YA WANAFUNZI, ELIMU YA CHINI KABISA, VYOO VICHAFU, LECTURERS WABABAISHAJI NA WANAFUNZI PIA. HUO NDO UKWELI WOTE. Kumbuka I am also a graduate wa pale

Huenda unayosema ni kweli lakini mbona hivyo vingine vizuri havipo kwenye ranking? Au tukubaliane kwamba Tanzania tuna Chuo Kikuu kimoja tu ambacho ni kichafu, elimu yake iko chini, ukimwi, lecturers wababaishaji n.k. Vingine ambavyo havina ukimwi, lecturers wababaishaji na elimu ya chini si vyuo vikuu bali shule za secondary ambazo zinajiita vyuo vikuu?

Kushuka kwa UDSM kwny hiyo Rank kwachangiwa na sababu zisizopungua 3 kuu.
1.SIASA
Kuanzia chuoni UDSM mpaka serikalini, UDSM pamekua jikwaa la siasa Ukada ndio umekua Ukada. Wewe kama sio wa magamba basi wa magwanda, tumesahau wanafunzi kilichotuleta pale. Pamoja na hayo tumekua chachu ya kutatua matatizo ya wanachuo nchini ila kudeseka kumepungua mno.
2.WAALIMU
Kua mwalimu asiena mapenzi ya dhati na kazi yake, prof. kaweka siasa mbele+ujasiriamali hapo hujachanganya mbinu mbovu za ufundishaji basi tunatengeneza bomu la Hiroshima.
Wengi wa waalimu wa UDSM ni source ya stress kwa wanafunzi, wengine ni kopy paste madesa na wengine mwanafunzi akija na ki2 kipya basi amekosa. Tatizo la kutuletea waalimu based on 1st class GPAz za madesa inatukost mno..
3.WANAFUNZI
Mitaala ya course za chuoni haijatulia kabisa,system ya ufundishaji na kupimia wanafunzi yatupeleka kua watu wa madesa oriented.mzazi wangu kaniambia nikasome nifaulu vizuri,nimefika UDSM CoET nakutana na mafunzo ya uhandisi yanihitaji nikariri zaidi ya kuelewa ili nisifeli.
Mpango wa kila mwanafunzi alomaliza fom 6 asome chuo kikuu inatukost pia,mwaka wa masomo uliopita UDSM wameletewa 1st years zaidi ya 5000 mara mbili ya mwaka wa masomo uliopita. Hapo ni kuleta vilaza na hata wanaostahili kua katika hatari ya kutoka vilaza pia.
Hatuko siriaz na masomo, starehe zimekithiri UDSM hakuna atakayenibishia katika hili.hata kama mtoto wa mkulima,hakuna ROHO kongwe ROHO isiyopenda mazuri basi hapo ndio twapotea kabisa kielimu kwa kuendekeza ujana.
4.SERIKALI
Zilianza shule za kata matokeo yake wahitimu wa elimu ya kidato cha nne wameongezeka na walioelimika na elimu hiyo ya kidato cha nne wanapungua siku hadi siku. Sasa naona serikali imehamisha majeshi Elimu ya juu, idadi ya vyuo vikuu TZ inaongezeka kwa kasi ya ajabu.kisa ni nini?!mtoe elimu mbovu tushindwe kushindana kwenye soko la ajira?!tuzidi kua wajinga ili mtutawale vyema?!elimu ya Chuo kikuu Tanzania yazidi kudharaulika je wa kulaumiwa nani kama sio serikali na mipango mibovu ya elimu!!TCU+HESLB ni mwiba kwenye elimu ya juu Tanzania,na tutazidi kuporomoka kielimu kama serikali haitajirekebisha.

Hitimisho:
Nina mengi sana ya kusema ila niishie hapo uhondo wa ngoma uingie ndani ucheze,naona wana JF wenzangu wanakoment kuhusu topic na naona wengine wanasema tu ya kuona na kuyasikia juu ya UDSM.Jamani jamani niliye ndani huku kwa muda huu naona uhondo wake,inasikitisha sana ila nitafanyaje maana machozi yangu yaweza fanana na samaki.
Huo hapo juu ni mtazamo wangu mwanafunzi wa UDSM niliekuepo UDSM toka 2008 mpaka sasa.

Nadhani haya ndio matunda ya Taifa kutokuwa na vipaumbele na serikali kuongoza nchi kwa ushabiki.

Yaani katika Top 100 Tanzania tuna Chuo kimoja tu? Khaa ina maana hivi vingine tunaviita vyuo vikuu ni Nursery?

evidence unayo hapo nilipo board!!!?

suluhisho la uliyo ya taja ni ipi!!!!?

Mkandala ndo tatizo

Mkandala ndo tatizo

mkandala ndo tatizo

ameacha kushughulikia mambo ya chuo, inauma sana

mbona cjaona udom! Au chenyewe ni chuo kikubwa na co kikuu!

suluhisho la uliyo ya taja ni ipi!!!!?

Nimeainisha posibo sababu as to why tumeshuka kwenye ranks ndgu HOYANGA..ni jukumu letu wana JF kuainisha na ikiwezekana kutolea posibo solutionz..hata wewe baada ya kusoma nilichoandika waweza toa suluhisho, maoni kipi kifanyike kwa maana sasa ushapata picha linganifu na muonekano wangu juu ya chuo changu.karibu ndugu.

Hahah..

Sikushangai.. jina lako linakusadifu wewe ni mtu wa aina gani!

Kwa Tanzania sioni chuo chochote chenye quality ya UDSM

madudu yaleyale

[TABLE="width: 570"]
[TR]
[TD="width: 570, bgcolor: #eeeeee"]Rank of Universities of Tanzania, United Republic of [/TD]
[TD="width: 1, align: right"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 570, colspan: 3"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 570"]
[TR]
[TD][TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: nav6a, colspan: 7, align: right"]First | Previous | Next | Last | Universities 1 to 6 of 6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD="colspan: 3"] [/TD]
[/TR]
[TR="class: bs5"]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD="colspan: 4"]POSITION[/TD]
[/TR]
[TR="class: bs5"]
[TD][/TD]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[TD="bgcolor: #cecece, colspan: 4"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: bs5"]
[TD]WORLD RANK[/TD]
[TD]UNIVERSITY[/TD]
[TD] [/TD]
[TD] SIZE[/TD]
[TD] VISIBILITY[/TD]
[TD] RICH FILES[/TD]
[TD] SCHOLAR[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD="colspan: 2"] [/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]3438[/TD]
[TD]University of Dar Es Salaam [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]2,589 [/TD]
[TD]4,395 [/TD]
[TD]3,962 [/TD]
[TD]4,024 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]8427[/TD]
[TD]Sokoine University of Agriculture [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]7,901 [/TD]
[TD]8,211 [/TD]
[TD]8,990 [/TD]
[TD]7,229 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]8819[/TD]
[TD]Hubert Kairuki Memorial University [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]6,113 [/TD]
[TD]8,872 [/TD]
[TD]13,382 [/TD]
[TD]6,048 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]9335[/TD]
[TD]Open University of Tanzania [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]9,430 [/TD]
[TD]11,149 [/TD]
[TD]6,533 [/TD]
[TD]7,229 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]10107[/TD]
[TD]Mzumbe University [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]5,903 [/TD]
[TD]11,877 [/TD]
[TD]12,286 [/TD]
[TD]7,229 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR="class: nav6a"]
[TD]11191[/TD]
[TD]Muhimbili University College of Health Sciences [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]12,641 [/TD]
[TD]10,885 [/TD]
[TD]9,048 [/TD]
[TD]7,229 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 7"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: nav6a, colspan: 7, align: right"]First | Previous | Next | Last | Universities 1 to 6 of 6[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
IMPORTANT: For each country only the Higher Education Institutions ranked in the top 12,000 positions are included. Complete coverage is over 20,000 organizations, The Catalogue's full list could be checked in the Directory by Country
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…