UEFA kwenye ubora wao kikosi bora cha msimu

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
11,880
Reaction score
10,372
2017–18 UEFA Champions League - Wikipedia

- Leo messi yumo ndani ya champion league squad of the season mbele ya Mane.
kuna kipi alichomzidi kwa mwaka huu? magoli ? timu kuifikisha mbali?

- Radja Nainggolan na James Milner pia hawamo kwenye kikosi badala yake James Rodrgous na Caseemiro wamekula shavu.
Hivi Milner amevunja record ya assist ndani ya champion league ya mwaka huu sijambo lakawida kabisa. jamaa kafanya kazi msimu huu na anasthili sifa yake. Na Nainggolan jamaa kakivuruga kabisa toka ligi inaanza mpaka semi final, mechi zote siza Barce, Liverpool, Chealse, Atletico, Shaktar jamaa kakamua kinoma.

Varane na Van Dijk hawakustahili kabisa kuwemo kikosini mbele ya Fazio na Kolarav. Jamaa wamepiga mpira waukweli kabisa.

Ila sikushangaa sana baada yakugundua katika committee ya kuchagua walikuemmo akina David Moyes.

Roma na Liverpool zimecheza vizuri sana mwaka huu na hasa Roma hata kama hazikua mabingwa. Wachezaji wao wamecheza kwa kiwango kikubwa sana.
 
Hii squad of the season ni upupuuuuu. Ukisoma maelezo ya kila mchezaji hapo unajiuliza imekuaje hata Mane kaachwa,?
 
Nimewshangaa sana
Messi na James hawakustahili kuwepo labda kama walikuwa wana angalia watu maarufu siyo mengine
 
Upangaji siku hizi umekuwa usanii mtupu hauzingatii vigezo nashangaa Radja Naingollan hayumo duuh hiyo ndo UEFA bhana.
 
Rodriguez msimu huu kapiga mpira mkubwa sana tuacheni masihara.. Messi uwezo wake still ni unquestionable labda hao waliobaki ila Messi na Rodriguez wamestahili
 
Rodriguez msimu huu kapiga mpira mkubwa sana tuacheni masihara.. Messi uwezo wake still ni unquestionable labda hao waliobaki ila Messi na Rodriguez wamestahili

hivi mkuu wewe unahisi messi kapiga mpira mkubwa zaidi ya MAne kwenye UEFA msimu huu?
N pia unahisi Rodrigues kapiga mpira mkubwa kuliko Nainggolan ?
 
Yani ulipomsifia milner eti kisa amepiga assist nyingi ndipo ulipoonyesha uelewa mdogo wa mpira!

Yani beki awekwe kwenye team of the season kwa sifa ya kutoa assist?

Mkuu, sifa ya beki ni kuzuia mashambulizi dhidi ya team yake, hayo mengine ni ziada.

Milner was outstanding on the UCL final, ila siwezi kumpa nafasi mbele ya Casemiro.

Kule watu wanaangalia namna unavyotimiza majukumu yako, sio sifa zisizokuhusu!
 
Rodriguez msimu huu kapiga mpira mkubwa sana tuacheni masihara.. Messi uwezo wake still ni unquestionable labda hao waliobaki ila Messi na Rodriguez wamestahili
Messi ana uwezo mkubwa sana sisi tunasema katika UEFA mwaka huu kachangia nini? hatujadili uwezo kwa maana nyingine unasema nafasi ipo tu hata kama hatacheza vizuri bali ni kwa sababu alikuwa. 2017/2018 je alistahili?
 
hakuna anaye pinga uwezo wa Messi
Ila UEFA ya 2017/18 hakistahili kuwepo kwa kikosi bora.
 
Messi ndiye mfungaji bora wa ulaya nzima hakuna mchezaji aliye mzidi kwa magoli toka katika ligi zote... una muachaje? ukishangaa hili nenda kashangae la Neymer kuwa mchezaji bora wa Lg1 ufaransa...
 
Huwa mnasahau tu, lakini pia udhamini wa Adidas huwa unamata sana na kumbeba Messi.
 
Adidas wanaidhamini Uefa.
Adidas wanamdhamini Messi na James.
Hivyo basi Uefa na Adidas na Messi ni chanda na pete.
Anhaa! Hiyo inaitwa rigging kwa kweli!
Messi ni mchezaji mkubwa na bora kuto mueka kwenye kikosi kusinge ondoa ubora wake hata kdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…