UEFA Super Cup 2018: Kwanini Atletico Madrid atashinda

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za mchana wana JF leo usiku kuna fainali ya kukata na shoka kati ya mabingwa wawili mmoja wa Europa league yaani Atletico madrid ya Hispania na mwingine champions league Real Madrid wa hispania pia ili kutafuat mbabe mmoja wa ULAYA na pua kuashiria kufunguliwa msimu mpya wa UEFA.


Kete zangu naipa Atletico kubeba ubingwa na hii ni kikubwa kwa sababu zifuatazo.

1. KIKOSI KIPANA
Atletico msimu huu imeunda kikosi imara kwa kuwa na wingi wa wachezaje wenye ubora kuzidi msimu uliopita ambapo hawakuruhusiwa kusajili na pia waliuza wachezaji wengi hivyo kujikuta wachezaji hawafiki 18 mwisho wa siku wanachoka mapema,kuumia,morale inashuka na mengineyo ila msimu huu kawasili Rodri,Arias,Martins,lemar,adan pamoja na kalinic hivyo kufanya kila mchezaji wa kikosi cha kwanza kuwa na sub yake hivyo wanakuwa match-fit na hali hii itawapa shida madrid na miamba mingine msimu huu.

2. UKUTA IMARA

Atletico ni timu yenye ukuta Imara ulaya nzima kwa misimu kadhaa sasa maana imefungwa magoli machache mno kuliko timu zote kwenye ligi zote kubwa. Mfano msimu uliopita iliruhusu magoli 22 pekee kwenye ligi huku Madrid wakiruhusu magoli 44!!!. Ukuta huu unasimamiwa na mzee mzima Diego Godin akisaidiwa na mzoefu savic hapo kati huku makinda wenye ubora wa hali ya juu yaani Jose Gimenez wa uruguay na Mshindi wa world cup Lucas hernandez wakiwa replacement. Upande wa kulia kuna santiago arias aliyekuwa mchezaji bora wa Ligi ya uholanzi huku akisaidiwa na mkongwe Juanfran, upande wa kushoto yupo beki mzoefu Felipe Luis wa brazil ambaye hana mpinzani kwenye namba yake kiasi theo amehamia Real madrid na lucas kahamia central back. Pia bila kumsahau golikipa bora wa misimu 4 mfululizo yaani Jan Oblak ambaye anaongoza kwa kuokoa michomo mikali na kufungwa magoli machache, hivyo kwa uwepo wake madrid watapata tabu mno.


3.DIEGO SIMEONE

Huyu pia ni sababu nyingine atletico watakuwa tishio msimu huu hasa wakikutana na madrid leo usiku. Kocha huyu tangia atuwe Atletico kaibadilisha timu na kuifanya ya kupambana sana hivyo watarajie moto huo kuongezeka msimu huu. Tumeona jinsi alivyowakuza vijana wadogo wasio na majina kma Thomas,correa,saul,koke,gimenez na lucas ambao kwa sasa wamekuwa wachezaji wa kuaminika kwenye timu zao za taifa, hivyo kwa uwezo wa kocha huyu lazima atletico itakuwa tishio kwa madrid leo usiku.

4. KIKOSI IMARA
Atletico inatengenezwa na wachezaji wasio na majina ila wanaojituma sana kitu ambacho kinawapa nguvu uwanjani. Ubora wa defence ukichangiwa na uimara wa midfield hasa uwepo wa Rodri koke na saul pale katikati wakisaidiwa na lemar kushoto na vitolo kuria watawapa challenge sana midfield ya Real madrid maana midfield ya atletico inatengeneza ugumu wa timu pinzani kupenya kwenye ngome yao. Uimara wa Atletico upo pia kwenye forward line yao ikiongozwa na Griezmann,diego costa na kinda machachari angel correa bila kumsahau mchezaji mpya Nikola kalinic aliyetoka Milan ambao wote wako vizuri kwenye umaliziaji hivyo kila chance watakayoipata leo inaweza kuwa maumivu kwa madrid

5.MFUMO WA UCHEZAJI

Atletico madrid inacheza mfumo wa kawaida wa 4-4-2 (Holding) ambapo midfield inacheza mchezo wa kujihami zaidi kuliko kushambulia hivyo kucontrol mchezo hapo kati na kutegemea counter attack chache kutafuta magoli na hii inaelezea kwanini msimu uliopita walishinda mechi nyingi kwa 1-0 maana walitumia muda mrefu kukaba na kutafuta fursa chache za kufunga na kurudi kukaba. Staili hii inawafanya wawe imara kwenye kukaba,kupasi,kumalizia na mwisho wa siku kuzuia mashambulizi ya timu pinzani. Na kwa uwepo wa mmoja wa washambuliaji bora duniani yaani costa+griezmann huku nyuma wakiwa na ukuta bora kabisa duniani Godin+Gimenez tunaweza shuhudia ushindi mwembamba lakini wa uhakika yaani unazuia magoli kupitia beki imara na unafunga goli kupitia striker imara.

Yote kwa yote mambo yataamuliwa leo usiku huko Talinn


#AupaAtleti
 
Naunga mkono hoja zako lakini pia ujue mpira dakika tisini.

Real nao kwa upande wao hawapo vibaya. Japo nami natupa karata yangu kwa Mhuni Diego Simione
 
Historia inawahukumu real Madrid kwamba huwa hawawezi kuendana na kasi ya mpira wa kihuni wa atletico Madrid.

Na Real kwa kutokuwepo their most influential player Ronaldo basi wanajiweka katika hali ya kukalia kuti kavu na hivyo kudondoka kwao hakutashangaza sana.
 
On fire
 
Aah always Los blancos huwa hapewi nafasi kwenye finals nyingi ila mwisho tunaona real anachukua...game ya usiku real anachukua hii ndoo trust me
Kumbuka aliyewabeba kasepa sidhani kama hawa watoto waliobaki wanaweza kutengua beki za atletico..... Anyway muda utaongea
 
Real madrid haijawahi kukubalika hata final ya UEFA mlisema hvihvi endeleeni na maneno yenu
Hahahaha hii ni Atletico sio wale majogoo wa karatasi kumbuka hata hapo bernabeu kwenye ligi hamjawahi kumfunga atletico kwa misimu 7 sasa!!! Kazi mnayo leo usiku tena sio ya kitoto
 
Mim Leo nmempa Madrid win simply because sjaona hatari yoyote kwa madrid....in terms of griezmn huyu hatafnya ktu kdogo costa mark my words atletico anakufa na hana ushindani kwa Madrid....muhindi anataka atuchanganye watu ila kazi ataiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…