UEFA Super League ni nini?

UEFA Super League ni nini?

mikedean

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
3,267
Reaction score
4,634
Uefa super league ni wazo la miaka ya 1990 ambayo baadhi ya vilabu vikubwa vilipendekeza kucheza wenyewe kwa wenyewe kwenye jumla ya timu 16 kubwa.

Uefa na Fifa walipinga vikali suala Hilo kwa mafai kwamba litaharibu ushindani wa ligi za ndani.

Lakini klabu za manchester united, chelsea, Arsenal, livapool, Juventus, Real Madrid Barcelona etc zimekubali kujiunga ligi hiyo lakini timu za Ujerumani bado hazijakubali moja kwa moja.

Eufa wamepigwa mkwara kwamba vilabu vitakavyokubali kucheza ligi hiyo Kama ligi hiyo itarasimishwa basi vinaweza kufutiwa usajili na wachezaji watakao cheza watapewa zuio la kuhamia kucheza ligi nyingine.

Je, klabu hizi kubwa zinaweza kufutiwa usajili?Hasara ni kwa Nani wakifanya hivyo? Je, kwa Nini Euefa wanaogopa ligi hii kwa kisingizio Cha kushuka kwa Uefa? Kwanini watu wengi kama wanaipinga. Je, lengo la mpira si ni kutengeneza pesa?sasa Kama timu zinapata pesa Tatizo liko wapi?kwa nini kuna Uefa nations league na Euro league?

Hebu tusaidiane michango Mawazo na tuelimishane umuhimu na hasara ya hii ligi.kisha tuwe na mzani inafaa au haifai kwa sababu

Karibu kwa michango[emoji120][emoji120][emoji120]
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hapo kuna masilahi ya watu.

Clubs zinaona UEFA wanafaidi sana kupitia juhudi zao. Hivyo wakianzisha LIGi yao watapata fedha zaidi kuliko kuwa kwenye CL.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kuna masilahi ya watu.

Clubs zinaona UEFA wanafaidi sana kupitia juhudi zao. Hivyo wakianzisha LIGi yao watapata fedha zaidi kuliko kuwa kwenye CL.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini Kama naona kuna ubinafsi wa Uefa humo, kwa sababu Uefa walianzisha Uefa nations league ambayo haikuwepo, sass kama mashindano haya hayaathiri Uefa champions league basi wakubali challenge
 
Acha yaanze na wao waongeze mapato,hizi timu kubwa za europe zinawekeza mkwanja mrefu kwenye timu zao.
Ndio hapo sasa , kikubwa kima mtu asiathiri Cha mwenzake, England kuna FA na Carabao na ligi lakini haziathiriani. kea hiyo hapo wakubali tu. Halafu nahsi FIFA wanaweza kuwageuka Uefa na kusapoti haya mashindano.
 
Ujio wa European Super League(ESL) , utafifisha uwepo wa UCL. Atletico, Tottenham, Liverpool, Real madrid, Barcelona, Inter & Ac milan, Juventus, Manchester city and United, Chelsea, Arsenal.

Bado kuna 3 teams zinategemea ku-confirm kushiriki kabla mwisho wa misimu hii ya 2020/2021.

Hizi ni Founding clubs kwaiyo ni must participants kwenye hii special league, still pia kutakua na vilabu kama vitano ambavyo vitapambana kufuzu ili kushiriki hii ligi.

It's all about money now.

Ikiwa hivi utamu wa UCL unatoka wapi?
 
Ni Ligi Kuu ya Ulaya ambayo ni mashindano mapya yanayoshirikisha vilabu 20 - na 15 vya kudumu, vinaitwa "vilabu vya waanzilishi " - na timu tano za wageni ambazo zitachaguliwa kuhusika kila msimu kulingana na matokeo ya misimu yao ya ndani ya ndani.

Super League imesema kwamba mechi zake zitafanyika katikati ya wiki, nafasi ambayo kawaida imehifadhiwa kwa mechi za Uropa kwani michezo ya nyumbani inachezwa wikendi.

Maono ni kwamba Ligi Kuu itachezwa kwa wakati mmoja na mashindano ya ndani kama Ligi Kuu - kama Ligi ya Mabingwa imekuwa ikichezwa - lakini kuna wasiwasi kwamba vilabu vya juu vitakuwa na nia ndogo ya kufanya vizuri kwenye ligi zao kwa sababu ya kudumu kwa ushiriki wao kwenye Super League.

Asili ya ligi za ndani ni kuzaa ushindani wa nafasi ya Ligi ya Mabingwa, lakini na Super League, hiyo inakuwa haina maana.

Vilabu vya waanzilishi vitahakikishiwa - kwa njia ambayo bado haijafafanuliwa - uhakika wa kushiriki katika mashindano tajiri zaidi (na kwa hakika ya kifahari), bila kujali matokeo yaliyopatikana uwanjani kwenye ligi zao za ndani. Hii, basi, ingeweza kupingwa na vilabu vingine.

Taarifa ya vyombo vya habari vya Super League ilisema kwamba ina mpango wa kuanzisha mashindano "haraka iwezekanavyo".

Mashabiki wengi, wachambuzi wa soka na taarifa za awali za UEFA &FIFA wameonekana kutokubaliana na ligi hii. Watu maarufu na wachezaji wa zamani wa vilabu husika wameonekana wakikosoa mashindano haya yanayotaraji kuanza mwezi August.
 
Uefa super league ni wazo la miaka ya 1990 ambayo baadhi ya vilabu vikubwa vilipendekeza kucheza wenyewe kwa wenyewe kwenye jumla ya timu 16 kubwa.

Uefa na Fifa walipinga vikali suala Hilo kwa mafai kwamba litaharibu ushindani wa ligi za ndani.

Lakini klabu za manchester united, chelsea, Arsenal, livapool, Juventus, Real Madrid Barcelona etc zimekubali kujiunga ligi hiyo lakini timu za Ujerumani bado hazijakubali moja kwa moja.

Eufa wamepigwa mkwara kwamba vilabu vitakavyokubali kucheza ligi hiyo Kama ligi hiyo itarasimishwa basi vinaweza kufutiwa usajili na wachezaji watakao cheza watapewa zuio la kuhamia kucheza ligi nyingine.

Je, klabu hizi kubwa zinaweza kufutiwa usajili?Hasara ni kwa Nani wakifanya hivyo? Je, kwa Nini Euefa wanaogopa ligi hii kwa kisingizio Cha kushuka kwa Uefa? Kwanini watu wengi kama wanaipinga. Je, lengo la mpira si ni kutengeneza pesa?sasa Kama timu zinapata pesa Tatizo liko wapi?kwa nini kuna Uefa nations league na Euro league?

Hebu tusaidiane michango Mawazo na tuelimishane umuhimu na hasara ya hii ligi.kisha tuwe na mzani inafaa au haifai kwa sababu

Karibu kwa michango[emoji120][emoji120][emoji120]
Hii ligi imeondoka na kibarua cha mourinho
 
Back
Top Bottom