Uelewa mdogo wa wananchi kudhoofisha harakati za upatikanaji wa Katiba Mpya

Uelewa mdogo wa wananchi kudhoofisha harakati za upatikanaji wa Katiba Mpya

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Matamanio ya watanzania wengi ni kuwa na katiba bora itakayoweza kusimamia rasilimali za nchi na kuhakikisha zinamnufaisha kila mwananchi na kuwa na ustawi mzuri wa jamii.

Licha ya matamanio hayo uelewa wa neno katiba bado ni mdogo miongoni mwa wananchi wengi. Huenda hali hiyo ikawa ni kikwazo kwa wananchi kupata katiba wanayoitaka. Juhudi za kuipata katiba mpya zimeanza muda mrefu lakini zimekuwa zikikwamishwa na baadhi ya watu ambao wanahofia kupoteza maslahi yao.

Kenya wamefanikiwa kupata katiba nzuri ambayo kwa kiasi kikubwa inakidhi matakwa ya wananchi wa taifa hilo. Uelewa wa wananchi hao katika masuala ya sheria na katika umewaunganisha na kuwaweka katika muelekeo sahihi. Kenya inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye katiba bora Afrika.

Mathalani mchakato wa katiba mpya ulikwama katika Bunge la Katiba mwaka 2015 baada ya makundi yenye maslahi kuibuka na kuipinga Katiba ya Warioba ambayo ilibeba maoni mengi ya wananchi. Katiba hiyo ikabadilishwa na kunyofolewa baadhi ya vipengele muhimu kama tunu za taifa, ukomo wa Ubunge, mfumo wa serikali tatu na nguvu aliyonayo rais.

Kutokana na uelewa mdogo wa katiba, wanasiasa wameitumia hali hiyo kama fursa ya kuendelea kujinufaisha na kuyaweka kando maslahi ya wananchi na taifa.

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Twaweza (2017) juu ya Sauti za Wananchi unaonyesha kuwa wananchi wengi wamesikia kuhusu mchakato wa katiba lakini hawajui hasa maana ya katiba na majukumu waliyonayo katika kuhakikisha katiba inatekelezwa ipasavyo katika kupata haki za msingi.

“Asilimia 93 ya Watanzania wameshawahi kusikia kuhusu katiba, lakini kati ya hao, asilimia 58 hawafahamu katiba ni nini”, inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya uchunguzi ambapo wananchi 6 kati ya 10 hawajui maana ya katiba.

Capture.png



Zaidi, soma hapa => Uelewa mdogo wa wananchi kudhoofisha harakati za upatikanaji wa katiba mpya | FikraPevu
 
Kinachonishangaza ni kwamba inawezekana vp wananchi wakataka katiba mpya hali ya kuwa hata hawana uelewa juu katiba,hao watanzania kama wanauelewa mdogo sana kuhusu katiba ni ajabu kuweza kujua kuwa hii katiba ya sasa si bora na kuhitaji katiba bora.
 
Back
Top Bottom