Uendeshaji wa Biashara ya saluni ya kike ya kisasa

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Tumeona urembo unavoendelea kuwa hadhi na ni hitaji la watu wengi hasa wanawake,nitaelezea namna ya kuendesha biashara hii kisasa hata kma sio msusi vitu gani unatakiwa uvizingatie.

Kwanza biashara hii ukitaka uiendshe kisasa lazima utoe hudumña 4 muhimu ambazo ni
1. Pedicure and manicure(kucha na kuoshamiguu)
2. Makeup (urembo wa uso)
3. Hairdressing(kusuka na kutengeneza nywele)
4. Spa(massage na facial)

Unatakiwa uwe makini kwenye kuchagua eneo chagua eneo ambayo Lina mkusanyiko kias wa watu namaanisha lilichangamka.

Unatakiwa utafute vijana professional kwaajili ya kazi hii wanaoweza kufanya kazi Kwa weledi na ufanis
Hakikisha unaweza vifaa vya kisasa na na vyenye ubora Ili kuvutia wateja

UTOAJI HUDUMA

1. Hakikisha unatumia bidhaa Bora kabisa za nywele makeup rangi za kucha na bidhaa zote za spa kuepuka madhara Kwa watumiaji usifuate vitu cheap

2. Jitahid kutoa ushauri wa masuala ya urembo Kwa watejawako wenye changamoto mbalimbali Kwa ustaarabu na unyenyekevu

3. Zingatia usafi na kujali wenye matatixo ya kuafya hapa nazungumzia kutoshare baadhi ya vifaa has vyenye ncha Kali pia unaweza kujikuta unamtoboa mteja ambae ana kisukar ikawa shida lazima ujue kuwahumia kulingana na halizao

4. Hakikisha ofisi sio sehemu ya kutoa huduma za kifamilia wew na nduguzako mkahudumiwe Bure lipa unapohitaji huduma utajenga nidhamu hata Kwa wafanyakaz wako kutotumia vitu vya ofis bila mpangilio

5. Pokea malalamiko rekebisha kwawakati zingatia saluni sio danguro Wala sehemu ya umbea nidhamu iwepo na simamia Hilo

6. Ulipaji wa wafanyakazi utegemee na ufanyaji wao wa Kaz mnapatana kias atachoingiza na kiasi atacholipwa hii inahasishwa ufanyaji kazi Kwa ubora Ili ahudumie watejawengi zaidi apate pesa nzuri usiwe mbahili lipa wafanyakazi Kwa wakati...
Antonnia
Lovelovie
We just path
Depal
lennie
Bantu Lady haya mje mjazie nyamanyama
 
7. Kauli nzuri kwa mteja, kuanzia wewe boss mpk wafanyakazi.

Kuna saloon siingii sbb mpaka rangi wao ana kimdomo. Yan wanajiona masupastaaa kitaa nzima.

Nilipaka rangi saloon X
Siku ya kutoa nipake nyingine nikaenda kwao. Mpaka rangi wake ananiambia “una kucha nzuri, ila nani alikupaka rangi vibaya hivi? Sijui hajakutengeneza vizuri.. mambo mob

Nikamwambia we tulia fanya kazi yako. Et siku nyingine usiende saloon za vichochoroni, uwe unakuja kwa masta C.
Nikamwambia ndo unakaribisha hivyo mteja mgeni?
Mwenzake akaanza kumwambia anazingua.

Toka hiyo siku, ile saloon sijarudi.
Nikaenda kumuadithia shoga angu ofisini. Akanambia wale ndo zao, kuna siku wanakuwa na majibu mbaya mpk unashangaa. Akasema ye mwenyewe pale haendagi.

Kwahiyo kauli mbovu kwa wateja zinafukuza wengine. Hata kama mnatoa huduma nzuri, ukimtreat mteja vibaya na pesa ni yake ni atakimbia.
 
7. Kauli nzuri kwa mteja, kuanzia wewe boss mpk wafanyakazi.

Kuna saloon siingii sbb mpaka rangi wao ana kimdomo. Yan wanajiona masupastaaa kitaa nzima...
7. Kauli nzuri kwa wateja. Ni lini wanawake wameanza kuelewana na kua na kauli nzuri baina yao ?! Ebo !!

Wanawake hawajawahi na kamwe hawataelewana na kupatana kwa dhati. Yani ukiwaona kwa nje wanavyoitana "shosti, dear, mamie," bla bla mwenzake akitoka tu anamsonyaaaa na kumsema kwa ubaya atamsema kuhusu sura, amevaaje, mabwana zao nk. ke wana unafiki pipa zima baina yao.

Hakuna na kamwe hakutakua na urafiki wa dhati baiya ya wanawake
 
7. Kauli nzuri kwa mteja, kuanzia wewe boss mpk wafanyakazi.

Kuna saloon siingii sbb mpaka rangi wao ana kimdomo. Yan wanajiona masupastaaa kitaa nzima...
Kabisa dear kunawakati watu wanafeli hapo na ndio mwanzo wa Biashara kufa na kuanza kulalamika biashara sio nzuri kumbe mdomo ndo unatuponza hii ni kweli kabissa
 
Wanawake hawajawahi na kamwe hawataelewana na kupatana kwa dhati. Yani ukiwaona kwa nje wanavyoitana "shosti, dear, mamie," bla bla mwenzake akitoka tu anamsonyaaaa na kumsema kwa ubaya atamsema kuhusu sura, amevaaje, mabwana zao nk. ke wana unafiki pipa zima baina yao.
Shida ni kwamba
Mtu una rafiki ambaye na yeye ana marafiki zake ambao wewe sio marafiki zako 😂

Patamu hapo
Muhimu ni kuishi kwa akili, ukishindwa Be you, Be yourself.
 
Eish
Hapa hatuzungumzii urafiki.

Kauli nzuri kwa mteja, unataka ama hutaki. Kwa ustawi wa biashara yako ni lazima.
ok, labda niboreshe - hakunaga maelewano baina ya wanawake. Hili liko wazi kama uchi wa mbuzi kwa mfano mwanamke akienda bank yuko radhi ahudumiwe na teller wa kiume hata kama foleni yake ni ndefu zaidi ya teller wa kike.

Mwanamke mjamzito huomba azalishwe na daktari mwanaume na sio mwanamke. Bottom line ni kwamba hakunaga maelewano baina ya wanawake hiyo "kauli nzuri" haiaplay kwa viumbe ke wakikutana.
 
Tumeona urembo unavoendelea kuwa hadhi na ni hitaji la watu wengi hasa wanawake,nitaelezea namna ya kuendesha biashara hii kisasa hata kma sio msusi vitu gani unatakiwa uvizingatie.

Kwanza biashara hii ukitaka uiendshe kisasa lazima utoe hudumña 4 muhimu ambazo ni
1. Pedicure and manicure(kucha na kuoshamiguu)
2. Makeup (urembo wa uso)
3. Hairdressing(kusuka na kutengeneza nywele)
4. Spa(massage na facial)

Unatakiwa uwe makini kwenye kuchagua eneo chagua eneo ambayo Lina mkusanyiko kias wa watu namaanisha lilichangamka.

Unatakiwa utafute vijana professional kwaajili ya kazi hii wanaoweza kufanya kazi Kwa weledi na ufanis
Hakikisha unaweza vifaa vya kisasa na na vyenye ubora Ili kuvutia wateja

UTOAJI HUDUMA

1. Hakikisha unatumia bidhaa Bora kabisa za nywele makeup rangi za kucha na bidhaa zote za spa kuepuka madhara Kwa watumiaji usifuate vitu cheap

2. Jitahid kutoa ushauri wa masuala ya urembo Kwa watejawako wenye changamoto mbalimbali Kwa ustaarabu na unyenyekevu

3. Zingatia usafi na kujali wenye matatixo ya kuafya hapa nazungumzia kutoshare baadhi ya vifaa has vyenye ncha Kali pia unaweza kujikuta unamtoboa mteja ambae ana kisukar ikawa shida lazima ujue kuwahumia kulingana na halizao

4. Hakikisha ofisi sio sehemu ya kutoa huduma za kifamilia wew na nduguzako mkahudumiwe Bure lipa unapohitaji huduma utajenga nidhamu hata Kwa wafanyakaz wako kutotumia vitu vya ofis bila mpangilio

5. Pokea malalamiko rekebisha kwawakati zingatia saluni sio danguro Wala sehemu ya umbea nidhamu iwepo na simamia Hilo

6. Ulipaji wa wafanyakazi utegemee na ufanyaji wao wa Kaz mnapatana kias atachoingiza na kiasi atacholipwa hii inahasishwa ufanyaji kazi Kwa ubora Ili ahudumie watejawengi zaidi apate pesa nzuri usiwe mbahili lipa wafanyakazi Kwa wakati...
Antonnia
Lovelovie
We just path
Depal
lennie
Bantu Lady haya mje mjazie nyamanyama
Ukiwa na wateja saluni inalipa sana ila uwe makini kuifuatilia kwa ukaribu!
 
Back
Top Bottom