UENDESHAJI WA TIMU: "Timu yauza wachezaji 18 na kusajili mbuzi kumi"-Uturuki

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488

Ukata katika Uendeshaji wa timu muusikie hivyo hivyo!! Yamewakuta waendeshaji wa timu ya soka ya Gulspor, klabu kongwe nchini Uturuki, iliyoanzishwa mwaka 1954. Yaani yamewafika shingoni kiasi cha kulazimika kuuza wachezaji mahiri tena chipikizi kumi na nane ili waweze kununua mbuzi kumi kuimarisha uwezo wa uendeshaji wa timu hiyo, ili ipate mafanikio ya kuchukua ubingwa.

Mbuzi" waliosajiliwa "wakijiweka tayari kwa 'kupasha misuri' wakiwa na Rais wa timu ndugu Kenan Büyüklebleb.

Nisiwachoshe...! Jisomee mwenyewe habari kamili hapa chini:
====
Turkish football team Gulspor has sold 18 youth players and bought 10 goats in a bid to earn ‘extra money from milk sales’ which will be used to serve the club’s priority needs.
The team’s president Kenan Büyüklebleb said that the step to buy goats was dictated by lack of available finance as there is no essential governmental or sponsorship investment for Turkish youth teams performing in lower leagues.

We must have a constant income,” Büyüklebleb told CNN Turkey. “Funds are overloaded because there is no government or corporate group support for our clubs. We need to get more investment for the kids [competing for the club].”
The club earned 15,000 Turkish lira (almost $2,600) after selling 18 youth players and plans to have around 5,000 lira ($863) profit from milk sales to cover the club’s expenses.
We got 10 goats. It will be a source of income for the youngsters,” Büyüklebleb said, adding that he acted in the interests of the team. “We think that breeding goats is profitable. We have bought them to raise better young players.
We expect to have 4,000-5,000 lira profit. At the same time, the number of goats will increase. At the end of six years, we are planning to have 140 goats for the club,” he added.

Based in the city of Isparta, Gülspor is one of the oldest clubs in Turkey, founded in 1954.
---------------------------------------------------------------
==>> Chanzo Rt.com
 
Jaribu ipeleka hata Google Translate hii taarifa yako!.
Imeuza wachezaji ikanunua Mbuzi ili maziwa ya hao mbuzi wauze wapate faida kuendeshea club!. We unaileta kama vile mbuzi wamesajiliwa kucheza mpira!. ELIMU! ELIMU! ELIMU!
 
ELIMU! ELIMU! ELIMU!
Naam, ni kweli elimu elimu elimu,!!! bila kujua matumizi ya alama za kufungua na kufunga semi, lazima elimu, elimu, elimu itatupa taabu sana.

Asante sana mkuu kwa kupitia uzi wangu nitayafanyia kazi maoni yako siku nikianzisha uzi mwingine.
 
Hapa Tanzania kuna chama flani kinakimbiwa kila uchwao wahusika waige huu mfano walau zipatikane fedha za kuendesha chama mana ruzuku zikikata ndio basi tena.
 
Yangaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naam, ni kweli elimu elimu elimu,!!! bila kujua matumizi ya alama za kufungua na kufunga semi, lazima elimu, elimu, elimu itatupa taabu sana.

Asante sana mkuu kwa kupitia uzi wangu nitayafanyia kazi maoni yako siku nikianzisha uzi mwingine.
Hongera mkuu, kukubali ulipokosea ni jambo la kishujaa.
Ila Yanga habri inawahusu sana. Hiyo staili ya kutembeza bakuli haitawasaidia wakati huo huo mnaongeza matumizi.
Mlitakiwa mkubali kua mpo kwenye kipindi kigumu afu mgekuja na future plan ya kuraise income ya club
 
Mkuu mbona hujasema wanampango wa kukamua maziwa na kuyauza kwenye mnada ili mapato yatakayopatikana yaendeshee timu ? wamefanya jambo zuri kwasababu hao wachezaji muda wote huo wapo na hela haziingii, ni bora hao mbuzi wataingiza pesa,,,,, YANGA MKO WAPI ?
 
Nilijua mbuzi wamesajiliwa kucheza mpira, haya mkuu asante kwa taarifa. Hata hapa nyumbani timu kongwe ziige huu mradi
 
Nilijua mbuzi wamesajiliwa kucheza mpira, haya mkuu asante kwa taarifa. Hata hapa nyumbani timu kongwe ziige huu mradi
Timu kongwe za hapa mpaka akina 'cleverwealth' wakubali vinginevyo hakuna kinafanyika...mambo ya ajabu sana timu kongwe zinawafanyia mashabiki.
 
yanga msimu huu wataenda mwanza na mabasi ya abiria maana sizani kama wana hata uwezo wa kununua wese la kuweka kwenye lile basi lao.. wafuge kuku waanze kuuza mayai huenda ikasaidia
 
yanga msimu huu wataenda mwanza na mabasi ya abiria maana sizani kama wana hata uwezo wa kununua wese la kuweka kwenye lile basi lao.. wafuge kuku waanze kuuza mayai huenda ikasaidia
 
Yanga Kumbe Wamefata Mfano Wa Hawa Waturuki Ndiyomana Wakaamua Kujipatia Kipato Kwa Kufuga Vyura Pale Jangwani Kwa Ajili Ya Kuwauzia Wachina Kitoweo.
 
Jaribu ipeleka hata Google Translate hii taarifa yako!.
Imeuza wachezaji ikanunua Mbuzi ili maziwa ya hao mbuzi wauze wapate faida kuendeshea club!. We unaileta kama vile mbuzi wamesajiliwa kucheza mpira!. ELIMU! ELIMU! ELIMU!
Anaendekeza mila na desturi za yanga na simba kutembeza bakuli au kumnyenyekea mtu ndo timu isafiri au iende kambini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…