Uenyekiti wa Chadema hauwezi, urais wa Jamhuri ya Muungano Lissu atauwezea wapi?

Mr worldwide

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2017
Posts
348
Reaction score
740
Good morning people!

Inasemekana kwamba mwaka 2020 Chadema imepanga kumsimamisha Tundu Lissu kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya CCM ya Magufuli.

Inaleta walakini kama mtu anayejinadi kuwa na uwezo wa kuongoza nchi kushindwa kuongoza chama chenye wanachama milion 6 out 50 milions ya Watanzania wote.

Mtu asiye na uwezo wa kuongoza chama kidogo ataweza vipi kuongoza Watanzania wote wa bara na visiwani?

Tundu Lissu na Chadema kwa hili mmepotoka, kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya chama tungeona na kumpima Lissu kama anaweza au hawezi.

Lakini kwa kushindwa kwake kuthubutu kuchukua fomu na kugombea uenyekiti wa chama hakika hatakuwa na uthubutu wa kuchukua fomu pia kuwania urais wa Tanzania.

Kwa jinsi Mbowe alivyochokwa na wanachadema hiki kiti anaenda kupoteza tena kwa mtu ambaye si mwanachadema wa asili.

Mwambe ana hoja za msingi na kama demokrasia ndani ya chama ikishika hatamu basi sina shaka Mbowe atapigwa chini.

Hii ilikuwa ni nafasi adhimu kwako Tundu Lissu kukiongoza chama na baadae nchi.

Ombi kwa vyama vya upinzani, tusirudie kosa la mwaka 2015 hapo mwakani.

Kwa pamoja tuungane na tumsimamishe mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kutoka ACT Wazalendo kwani ndio saizi ya jiwe kwa sasa hapa nchini.

Tuwachane na akina Membe, hao mwishowe ni lazima warudi kwa baba na mama yao CCM.
 
Ambao si wanachadema, husema Mbowe amechokwa!
Hakuna mwa Chadema wa kweli mwenye shaka na uwezo wa Mbowe...
Mbowe ni mwiba kwa wapinzani wake wote, hasa maccm!
ACT 2020 hata diwani hawapati...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hii elimu inayotolewa na ccm kwa watoto wa Tanzania Mungu anaiona
 
Lissu ni mr vichekesho huyo

Hana lolote

Yeye abakie kwenye sheria tu siasa hawezi
 
Kama mtu aliyekuwa anasimamia barabara na madaraja na samaki sasa hivi anasimamia watu, je, kwa huyo aliyekuwa anawaongoza wasomi wanasheria si itakuwa jambo rahisi?
 
Hizi ni kande, mchanyato ama mseto!!! Lissu, Mbowe, Zitto, Membe, how!!?
Epuka mikorogo itakudhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…