Ufadhili wa masomo Tanzania

Ufadhili wa masomo Tanzania

Haph

Member
Joined
May 26, 2021
Posts
5
Reaction score
4
Habari wakuu,

Naomba msaada wa kimasomo kwa atakayeguswa ama anaefaham mashirika yanayotoa misaada ya kimasomo kwa ngazi ya cheti.

Natamani sana kuendelea na masomo ila hali ya kimaisha ndo changamoto kwangu nilifaulu kwenda form five nikasoma mpaka form six ila sikufanya mitihani yangu.

Kwa anaeweza kunisaidia hata Kama ni kwa maandishi naomba anisaidie pia Kama kuna mashirika yanayoweza kunisaidia kwa hapa Tanzania naomba anaefaham anisaidie natamani kuendelea na masomo ila uchumi ndo changamoto kwangu.
Hata msaada wa kimawazo jinsia ni female
Matokeo yangu ya form four yalikuwa:

Civics-D
History-C
Geography-C
Kiswahili-C
English-C
Physics-D
Chemistry-C
Biology-B
Mathematics-D

Asanteni.
 
Matokeo yako Ni mazuri Sana. Nakushauri Anza kuomba nafasi chuo Kwanza( Omba diploma in clinical medicine chuo Cha serikali, utapata kwani una ufaulu mzuri)

Ukipata barua ya admission chuoni nenda Kanisani/msikitini utachangiwa Ada. Hata hapa JF wako wadau watakuchangia

Kama hutojali , kwa Nini hukufanya mitihani ya kidato Cha sita?
 
Nakushauri usipote mda wako huko nenda pale DTI kuna short course za Petroleum and Gas piga zile ndio fursa ilipo uko

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Matokeo yako Ni mazuri Sana. Nakushauri Anza kuomba nafasi chuo Kwanza( Omba diploma in clinical medicine chuo Cha serikali, utapata kwani una ufaulu mzuri)

Ukipata barua ya admission chuoni nenda Kanisani/msikitini utachangiwa Ada. Hata hapa JF wako wadau watakuchangia

Kama hutojali , kwa Nini hukufanya mitihani ya kidato Cha sita?
Nilipata matatizo kiafya mkuu
 
Chukua ushauri hapo juu tafuta chuo kwanza na coz ya ndoto zako then Rudi hapa tukuchangie mie binafsi ikiwa utakidhi vigezo vya kupewa msaada Basi nitalipa gharama ada kwa miaka miwili.

Sio nitafanya hivi kwa ajili ya kutafuta sifa ila nimekumbuka Jambo gumu sana kuhusu member mmoja hapa Jf ( MPAUKO) nisamehe huko uliko😭😭😭
 
Sawa mkuu ntafanya hivyo
pia asante
 
Back
Top Bottom