Chama cha Mapinduzi
Member
- Aug 8, 2013
- 10
- 33
KARIBU KATIKA KUIJUA ILANI YA CCM 2015/2020 ILANI AMBAYO NDIYO MKATABA WAKO MWANANCHI NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA DR JOHN POMBE MAGUFULI:
ILANI YA UCHAGUZI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 KWA KUWACHAGUA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO, RAIS WA ZANZIBAR, WABUNGE, WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA MADIWANI IMEANDALIWA IKIWA NI MKATABA KATI YA CCM NA WANANCHI.
Katika kipindi cha Miaka mitano ya Utawala wa CCM ikiwa madarakani, itazielekeza Serikali zake (SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA) kuendelezana kupambana na changamoto kubwa NNE zifuatazo:
1. KUPAMBANA NA UMASKINI
Pamoja na Ongezeko la kukua kwa Uchumi na Ongezeko la huduma za kijamii, vilivyopatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Serikali ya Awamu ya Tano itazielekeza Nguvu zake katika kufanya mambo yafuatayo:
a. Kuhamasisha kilimo kuoitia kauli mbiu ya KILIMO KWANZA.
b. Kuongeza kasi ya kupima ardhi na kuwapatia wananchi HATI ZA KIMILA ambazo watazitumia kama dhamana katika kuomba mikopo na Kuendeleza shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
c. Kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma za kijamii kama ikiwemo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa nyumba bora; na
d. Kuongeza kasi ya kurasisha biashara na kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo maeneo ya kufanyia biashara na fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu.
2. AJIRA KWA VIJANA
Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana serikali ya awamu ya tano inategemea kuanzisha viwabda vidogo,viwanda vya kati na viwanda vikubwa ambavyo vitaweza kuajiri watu wengi na kuzalisha bidhaa za kutumiwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.
Katika kipindi cha 2015-2020, sekta ya uzalishaji mali kama kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda vikubwa na vidogo na huduma za kiuchumi kama vile miundombinu ya nishati, uchukuzi na ujenzi zitaelekeza mipango yao katika kupunguza umaskini na kuanzisha ajira hususan kwa vijana. Aidha huduma za kijamii za elimu, afya na maji zitajielekeza kuondoa umaskini na kuongeza ajira.
3. Vita dhidi ya rushwa
Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii hazitaleta manufaa kwa wananchi na kuondoa umaskini iwapo adui RUSHWA ataendelea kulitafuna taifa letu.
Katika Miaka mitano, CCM itapambana na Rushwa na kuziba mianya yote ya Rushwa katika Taasisi za Umma, kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza Rushwa Serikali na katika Sekta Binafsi. Tutaimarisha vyombo vya kuzuia na kupambana na Rushwa ikiwa ni pamoja na KUANZISHA MAHAKAMA KWA AJILI YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI.
PAMOJA NA KUPAMBANA NA RUSHWA SERIKALI ITASHUGHULIKIA KWA UKALI ZAIDI TATIZO LA UBADHIRIFU NA WIZI WA MALI A UMMA, KUCHELEWESHA KUTOA MAAMUZI YENYE MASLAHI KWA UMMA NA KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MASUALA YENYE MASLAHI KWA UMMA.
4. ULINZI NA USALAMA
NCHI YETU IMEKUWA KWENYE UTULIVU TANGU KUPATA UHURU MWAKA 1961 NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MWAKA 1964. IMEKUWA KIMBILIO LA MATAIFA YENYE MIKWARUZANO NA MSURUHISHI WA NCHI MAJIRANI. LAKINI SIKU ZA HIVI KARIBUNI KUMEONEKANA VIASHIRIA VINAVYOLETA HOFU KWA USALAMA KWA WANANCHI WETU HASA VITENDO VYA MAUAJI YA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO), KUUAWA KWA VIKONGWE, UKATILI RIDHI YA WANAWAKE NA WATOTO NA TISHIO LA VITENDO VYENYE MWELEKEO WA KIGAIDI.
KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO, CCM ITAZIELEKEZA KUENDELEZA NA KUIMARISHA VYOMBO VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA KWA KUVIONGEZEA RASLIMALI FEDHA, RASLIMALI WATU, MASLAHI, ZANA ZA KISASA NA MAFUNZO.
AIDHA ELIMU KWA UMMA ITATOLEWA ILI KUONDOA IMANI POTOFU ZA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA VITENDO VYA MAUAJI YA MAKUNDI HAYO.
KARIBU KATIKA KUIJUA ILANI YA CCM ......
ITAENDELEA SEHEMU YA PILI, NA NI MWENDELEZO WA ELIMU YA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI