Elections 2015 Ufafanuzi: Ilani CCM 2015-2020 (Sehemu ya I)

Joined
Aug 8, 2013
Posts
10
Reaction score
33
KARIBU KATIKA KUIJUA ILANI YA CCM 2015/2020 ILANI AMBAYO NDIYO MKATABA WAKO MWANANCHI NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA DR JOHN POMBE MAGUFULI:

ILANI YA UCHAGUZI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 KWA KUWACHAGUA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO, RAIS WA ZANZIBAR, WABUNGE, WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA MADIWANI IMEANDALIWA IKIWA NI MKATABA KATI YA CCM NA WANANCHI.

Katika kipindi cha Miaka mitano ya Utawala wa CCM ikiwa madarakani, itazielekeza Serikali zake (SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA) kuendelezana kupambana na changamoto kubwa NNE zifuatazo:

1. KUPAMBANA NA UMASKINI

Pamoja na Ongezeko la kukua kwa Uchumi na Ongezeko la huduma za kijamii, vilivyopatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Serikali ya Awamu ya Tano itazielekeza Nguvu zake katika kufanya mambo yafuatayo:

a. Kuhamasisha kilimo kuoitia kauli mbiu ya KILIMO KWANZA.
b. Kuongeza kasi ya kupima ardhi na kuwapatia wananchi HATI ZA KIMILA ambazo watazitumia kama dhamana katika kuomba mikopo na Kuendeleza shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
c. Kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma za kijamii kama ikiwemo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa nyumba bora; na
d. Kuongeza kasi ya kurasisha biashara na kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo maeneo ya kufanyia biashara na fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu.

2. AJIRA KWA VIJANA

Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana serikali ya awamu ya tano inategemea kuanzisha viwabda vidogo,viwanda vya kati na viwanda vikubwa ambavyo vitaweza kuajiri watu wengi na kuzalisha bidhaa za kutumiwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.

Katika kipindi cha 2015-2020, sekta ya uzalishaji mali kama kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda vikubwa na vidogo na huduma za kiuchumi kama vile miundombinu ya nishati, uchukuzi na ujenzi zitaelekeza mipango yao katika kupunguza umaskini na kuanzisha ajira hususan kwa vijana. Aidha huduma za kijamii za elimu, afya na maji zitajielekeza kuondoa umaskini na kuongeza ajira.

3. Vita dhidi ya rushwa

Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii hazitaleta manufaa kwa wananchi na kuondoa umaskini iwapo adui RUSHWA ataendelea kulitafuna taifa letu.

Katika Miaka mitano, CCM itapambana na Rushwa na kuziba mianya yote ya Rushwa katika Taasisi za Umma, kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza Rushwa Serikali na katika Sekta Binafsi. Tutaimarisha vyombo vya kuzuia na kupambana na Rushwa ikiwa ni pamoja na KUANZISHA MAHAKAMA KWA AJILI YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI.

PAMOJA NA KUPAMBANA NA RUSHWA SERIKALI ITASHUGHULIKIA KWA UKALI ZAIDI TATIZO LA UBADHIRIFU NA WIZI WA MALI A UMMA, KUCHELEWESHA KUTOA MAAMUZI YENYE MASLAHI KWA UMMA NA KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MASUALA YENYE MASLAHI KWA UMMA.

4. ULINZI NA USALAMA

NCHI YETU IMEKUWA KWENYE UTULIVU TANGU KUPATA UHURU MWAKA 1961 NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MWAKA 1964. IMEKUWA KIMBILIO LA MATAIFA YENYE MIKWARUZANO NA MSURUHISHI WA NCHI MAJIRANI. LAKINI SIKU ZA HIVI KARIBUNI KUMEONEKANA VIASHIRIA VINAVYOLETA HOFU KWA USALAMA KWA WANANCHI WETU HASA VITENDO VYA MAUAJI YA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO), KUUAWA KWA VIKONGWE, UKATILI RIDHI YA WANAWAKE NA WATOTO NA TISHIO LA VITENDO VYENYE MWELEKEO WA KIGAIDI.

KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO, CCM ITAZIELEKEZA KUENDELEZA NA KUIMARISHA VYOMBO VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA KWA KUVIONGEZEA RASLIMALI FEDHA, RASLIMALI WATU, MASLAHI, ZANA ZA KISASA NA MAFUNZO.

AIDHA ELIMU KWA UMMA ITATOLEWA ILI KUONDOA IMANI POTOFU ZA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA VITENDO VYA MAUAJI YA MAKUNDI HAYO.

KARIBU KATIKA KUIJUA ILANI YA CCM ......

ITAENDELEA SEHEMU YA PILI, NA NI MWENDELEZO WA ELIMU YA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

 
Mkuu endelea kutuelimisha na ilani hii,tutafurahi kujua mkataba wetu na ccm maana hamna namna
 
Kwangu bado imepwaya na haijielzi vya kutosha ni jinsi gani ya kupata hizo pesa za kuendesha kilimo, kulipa vijana watakaoajiriwa, ni kwa namna atapambana na rushwa, kuinua kilimo kwa njia zipi-soko au pembejeo, athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ilani hii itamsaidiaje mkulima?

Pia, rasilimali za nchi hazijaelezewa ni jinsi gani zitatumika kuinua pato la taifa, kodi bilabila
 
Kwa hiyo ilani hii ni mawazo ya kamati ya kampeni ya watu 30?
 
Kwenye sherehe ya blues unatuwekea sebene
 
1.kupambana na umaskini;

mngekuwa na nia kweli ya kupambana na umaskini msingeleta magumashi hivi karibuni kwenye mikataba yenu ya gesi mliyosaini juzi tena kwa dharula....

Mngekuwa na nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania na umaskini ungemwekea kwanza miundombinu bora ya kupata elimu lakini badala yake pesa zinaibiwa kila kukicha huku wazazi wakibwanwa kutoa pesa za maabara

kwa hili liko wazi mmeshindwa kwa kiasi kikubwa.

2. Ajira kwa vijana.

Hapa tena ndo hamtuambii kitu kabisaa
mmeuwa viwanda karibia vyotee kwa tamaa zenu za kujilimbikizia mali
hali imekuwa ngumu kwa vijana wengi huku mitaani
hatuwataki kabisaa bora tuwaondoeni madarakani tujaribu upande mwingine kwanza.....

3. Vita dhidi ya rushwa

''rushwa'' hii ndio imekuwa kama kauli mbiu ya ofisi za selikari siku hizi....
Sio kwenye kupata huduma za afya,elimu,ajira,leseni,usalama n.k
tumeshuhudia mabilioni yakichotwa mchana kweupeee na rais akadiriki kusimama adharani na kuuaminisha umma kwamba zile si fedha za serikali....tena kwa kutabasamu!
Hili kwa kweli mmelikumbatia kwelikweli na mnatudanganya mchana kweupee...mmeshindwa bora mpunzike kwanza.

4. Ulinzi na usalama

hatujasahau ya mwangosi wala ulimboka..... Migomo na vurugu kila kukicha..
Ndio ikumbukeni na kauli ya waziri mkuu pia ''wapigwe''
ulinzi na usalama umekuwa ni kwa ajili yenu tu watu wenye madaraka si kwaajili ya sisi watu wa chini.
Leo hii likitokea tatizo ukitoataarifa kituo cha usalama ndio kwanza utaambiwa utoe kitu kidogo, oooh mara gari haina mafuta..., tumewachoka!

Sehemu ya kwanza imeshafeli tayari hamna haja ya kuleta sehemu ya pili.

Mabadiliko...!
We need changes.
Tanzanians need changes.

 
Kabla hawajaleta Ilani nyingine watueleze in vipi au kwa kiasi gani wametekeleza ilani zilizopita, au wanafkiri wananchi tuna ubongo wa wa ndezi?? Miaka karibia 30 mantuahidi mtamaliza unaskini huo umaskini hauishi!

Acheni kucheza an akili zetu CCM mlitakiwa mwaka Huu mtuoneshe mlichofanya ili mchaguliwe sio kutuahidi tena.... Ndo mana hamna cha kutuonesha mnaishia kutuonesha push ups na wasanii...
 
Kabla hamjaenda mbali naomba mrekebishe uandishi. Kuandika sentensi nzima kwa upper case ni kumpa msomaji ugumu wa kusoma. Unaonekana kama unapayuka, na andiko linakosa flow. Ni utaalamu wa msingi kabisa wa maandishi...
 

Huu ni uandishi wa aina gani! Mna haraka gani mnashindwa kufanya editing walau mnachoandika kisomeke!
 

Kwani kabla ya hapo zilikuwa zinaelekezwa wapi?
 
Kabla hamjaenda mbali naomba mrekebishe uandishi. Kuandika sentensi nzima kwa upper case ni kumpa msomaji ugumu wa kusoma. Unaonekana kama unapayuka, na andiko linakosa flow. Ni utaalamu wa msingi kabisa wa maandishi...
Asante kwa ushauri, tutazingatia sana hili.
 
Ilani mnaitupa mkichaguliwa kama mlivyotupa rasimu ya katiba,CCM OUT
 
Kabla hawajaleta Ilani nyingine watueleze in vipi au kwa kiasi gani wametekeleza ilani zilizopita, au wanafkiri wananchi tuna ubongo wa wa ndezi?? Miaka karibia 30 mantuahidi mtamaliza unaskini huo umaskini hauishi
Asante sana kwa maoni haya.

Tutakuja na hoja nyingine juu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
 
Pia kuna typing errors nyingi sana...
Jitahidini kuandika kiswahili sahihi hususani matumizi ya R kwenye L
Tutazingatia, kwa kuanzia tutarekebisha hili bandiko la kwanza. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
 
Ccm mnajitahidi sana kuongea lakini mwaka huu yunataka tubadishe chama. Tumechoka na lichama lenu.
 
Nimependa sana hii. CCM inakuja kisasa zaidi. Ngoja tusubiri sehemu nyingine.
 
Hawa ni vibaraka wa CCM, Maendeleo ya kweli nchi hii kamwe hayataletwa na CCM, shime Watanzania tusiyumbishwe, wembe ni uleule CCM OUT..
 
Chama cha Mapinduzi

Lipeni deni kwanza, tuliyoahidiana kuwapa madaraka awamu zilizopita tufanye auditing, je mmetimiza ? kwa kiasi gani? kama hapana tutawaaminije kuwa mtatimiza? Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa mikataba.

Pili, Katibu Mkuu Kinana anatuhumiwa kutumalizia Tembo wetu, je hamuoni ni committing suicide kuwapa nafasi tena?

Tatu, imedhihirika Chama hiki kinalea impunity. Mfano, waliobeba mapesa kwenye lumbesa walificha, je mnajiona kuwa kuna legitimacy tena ya kuaminika?

Nne, 2010 Chadema walisema elimu hadi form four itakuwa bure, mkasema hizo ni porojo za Padre Slaa,lakini leo hii mmeiga na kusema inawezekana.

Sasa wenzenu UKAWA wanasema Elimu hadi Chuo kikuu ni bure ninyi mnasema haiwezekani,kwanini tusiwape madaraka hawa ambao ni creative, ili hiki chama ambacho ni chakavu kikatulie kijitathimini?

Tano,kwanini mnatumia nguvu nyingi, zilizohalali na haramu katika kampeni zenu? Je kwanini madaraka mnayataka kwa nguvu zote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…