Baada ya maneno mengi kuzungumzwa kuhusu mgawo wa pesa kutoka caf kwenda tff ,hatimae shirikisho limetolea ufafanuzi
View attachment 1633712
Pana mdau katoa maoni yake kama ifuatavo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Wilfred Kiadau amekiri kuwa Shirikisho la Soka barani Africa ambalo Rais wake amefungiwa na FIFA baada ya Kuwatumia Maraisi wa Mashirikisho pesa kupitia akaunti zao Binafsi zenye viashiria vya Rushwa.
Kama hivyo ndivyo Bwana Kiadu amekosea sana kwakuwa sasa anampaka matope Rais wa TFF bwana Karia kuwa Kweli Pesa hiyo Pound 20,000 ziliingia kwenye Akaunti Binafsi wakati SHIRIKISHO lina akaunti rasmi.
Kwa kukiri huku kwa Katibu Mkuu wa TFF anaweka bayana kuwa Rais Karia amepokea RUSHWA.
Aidha kwa maelezo ya Bwana Kidau ni kuwa Rais wake wa TFF bwana Karia alitoa pesa hiyo na kuiingiza kwenye matumizi ya kawaida ya Shirikisho hilo... Swali ni Matumizi yapi na kwa Tarehe ipi?? Na je Mtumaji alipotuma alituma kwa Akaunti Binafsi ya Raisi kwa Bahati mbaya au kwa Makusudi yapi.??
Kwa kitendo hiki cha kukiri kwa Bwana Kidau kinaleta Tafsiri kuwa RUSHWA hii kutoka kwa Rais wa CAF kuwahusisha watumishi wote wa TFF.
Kitendo cha kupokea na kuzifanyia matumizi kwa maslahi ya Tanzania maana yake pia ni kuingiza Taifa lote kwenye KASHFA YA RUSHWA inasikitisha sana.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa Hivi hadhi yetu Watanzania inaweza kuchafuka kwa Rushwa ya dola au paundi 20 000 elufu?
Je kwa kitendo hicho ni takwa la Serikali yetu,?
Je Serikali au Watanzania tulikwama kiasi cha sisi na serikali kuwa na uhitaji wa hiyo Rushwa ili shughuli zetu ziende??
Kama Rais anapokea na Katibu anakiri hadharani Je ndani ya shirikisho iliyogubikwa na vitengo vyake vya marefa na chaguzi tunategemea nini?
Kidau hakupaswa kukiri kwa kupokea Rushwa na kutuaminisha kwamba tumeingiziwa kwenye matumizi ya maendeleo.
Kwa hali hii na sintofahamu hii niliposoma kile kipande cha hukumu kimetaja neno TANZANIA imeniuma sana na kuumizwa Taifa letu kuchafuka.
Sitaki kusema katika mazingira haya TFF imetukosea Bali natamani kuona weledi wa uwajibikaji wa nafsi kwa tuhuma hizi kubwa Duniani.
BADO NINAUMIA.
WAKATI WA KARIA KUMFATA MALINZI UMEWADIA.>