Advocate_Silayo
Member
- Aug 5, 2019
- 64
- 93
Haki za binadamu ni swala ambalo haliwezi kukwepwa na binadamu yeyote yule Duniani. Ni haki ambazo kimsingi zina manufaa makubwa katika ustawi wa jamii nzima. Katika nchi yetu ya Tanzania haki hizi za binadamu zimeorodheshwa katika Katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara kuanzia Ibara ya 12 hadi 24.
Katika Ibara hizo Katiba yetu inazungumza mambo yafuatayo:
Ikumbukwe kwamba haki hizi kuu nne kama ambavyo mimi binafsi nimependa kuziita zina muunganiko wa moja kwa moja baina ya moja na nyingine (zinategemeana) yaani huwezi kuisema moja na kuiacha nyingineyo. Bhasi tuanze moja kwa moja na uchambuzi kuhusu haki hizi za binadamu huku tukihusianisha moja kwa moja na kuchochea maendeleo katika jamii zetu.
HAKI YA USAWA (Inapatikana kwenye Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya JMT
Kama vile ambavyo wewe binafsi hupendi kufanyiwa jambo baya katika maisha yako bhasi ndivyo hivyo hivyo unapaswa kumfikiria na mwingine. Dhana ya usawa katika haki za binadamu imeletwa kwa makusudi ili binadamu mmoja aweze kuona namna anapaswa kuishi kwa kuheshimu mwingine katika mambo mbali mbali. Kwanza kabisa binadamu wote tunazaliwa tukiwa huru na wote tukiwa sawa kisheria na kijamii, hatuzaliwi tukiwa tunabaguana kwa makabila wala lugha zetu tunazozizungumza,tunatambuliwa kwa heshima na utu wetu katika jamii nzima.
Lakini pia tunapozungumzia swala la usawa katika mambo ya kisheria mtu yeyoye yule hatoweza kupewa adhabu bila ya kujulikana kwa kosa lake kimahakama kwasababu Mahakama ndio chombo pekee katika nchi yetu chenye maamuzi ya mwisho katika utoaji wa haki na adhabu kwa mujibu wa sharia husika. Mwananchi huyo hata kama itatokea anafanyiwa uchunguzi iwe katika makosa ya jinai ama madai hatopaswa kunyanyaswa,kudhalilishwa ama kufanyishwa adhabu yoyote ile ambayo inatweza utu na heshima yake kama mwanadamu.
Sasa katika jamii yetu ya kitanzania tunaweza kabisa tukawa na jamii yenye usawa wa kibinadamu endapo tu tutaishi kwa kuheshimiana sisi kwa sisi hata bila ya shuruti ya kisheria ama vyombo vya ulinzi na usalama. Usawa unaanzia ndani ya familia yako ewe baba au mama wafundishe watoto wako upendo na kuheshimu watu wengine ambao sio wa familia yako, lakini pia kama wazazi wanapaswa kutowaonyesha magomvi yao kama wazazi kwa watoto maana wakishaona baba ana mpiga mama mpaka analia bhasi watoto wa kiume wataona ni sawa mama kupigwa na hawatasita kuwapiga wanawake wengine ambao sio mama zao waliowazaa, lakini pia mtoto wa kike ataona ni sawa kupigwa na mwanaume yeyote yule kwasababu mama yake alikuwa akipigwa na baba yake pasipo kusema lolote. Hali hizi huchangia malezi mabaya na huenda pia watoto hao wakaja kuwa viongozi wa kitaifa na wakayafanya hayo pasipo kuwa na uelwa mzuri na kuona wako sahihi kumbe wanakosea kijamii na kisheria pia,hivyo tuanzishe mabadiliko ndani ya familia zetu kwanza kama kweli tunahitaji ustawi mzuri wa Taifa letu la Tanzania.
HAKI YA KUISHI (Inapatika kwenye Ibara ya 14,15,16 na 17 ya Katiba ya JMT)
Lengo la kuzaliwa ni kuishi kwa amani na uhuru kama ambavyo watu wengine na hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mwanadamu yeyote yule. Hivyo bhasi kila mwanadamu anapaswa kuishi kwa uhuru na kujifanyia mambo yake katika faragha iliyo nzuri pasipo kuingiliwa ama kuzuiliwa na mtu mwingine.
Ukiwa kama mwanadamu mwenye afya na akili timamu katika kuishi kwako hutaacha kusafiri na kwenda maeneo mbalimbali ya nchi hii iwe ni kikazi,kimaisha ama kwa kutalii, na unafanya namna hiyo pasipokuwepo na bugudha ama katazo la aina yeyote ile kama mwanadamu huru. Ikumbukwe kwamba kuua mtu ni kosa la jinai lakini pia kumnyima mtu uhuru wa kwenda anakokutaka ama kuingilia faragha zake katika maisha yake ni kosa kisheria,hivyo binadamu huyu anapaswa kuwa huru na maisha yake lakini anatakiwa kuishi kwa uhuru na kwa kuzifuata sharia za nchi ili awe raia mwema.
Tunaweza kuyakomesha matendo ya mauaji katika jamii zetu kwa kufundishana kwamba uhai wa mtu huja mara moja katika maisha na unapomuua mwenzako bhasi jua fika ni kosa la jinai kisheria lakini pia ni dhambi katika Imani za kidini kwa maana ya Mwenyezi Mungu hapendwezi na jambo hilo,mtakubaliana na mimi kwamba endapo tutaishi kwa upendo na usawa hakutakuwa na mauaji ya binadamu wenzetu kwasababu kinachokufanya umuue binadamu mwenzako ni kwasababu huoni kama ni sawa na wewe na huoni kama anastahili kuishi kama wewe ulivyo.
Swali chonganishi: kwanini sasa bado Mahakama inatoa amri ya mtu kunyongwa mpaka kufa endapo akikutwa na kosa la mauaji kwa kukusudia?
Binafsi huwa nina mawazo tofauti kidogo na namna sheria inataka kwamba kumnyonga mtu aliyemuua mwenzake hakufanyi yule aliekufa kuhisi kwamba ametendewa haki kwasababu uhai wa binadamu haurudi mara mbili. Lakini pia ninaona kwamba tutazidi kujichukulia uhai wa watu wengine kwa kisingizo cha aliua mwenzake hapo kabla sasa itakuwa ni kama tunalipiza kosa la awali,lengo la adhabu ni kumfanya mhusika ajue kuwa kakosea hivyo akiuwawa pia hatojutia bhali akiwa jela maisha atajutia kosa lake.
HAKI YA UHURU WA MAWAZO (Inapatikana kwenye Ibara ya 18, 19, 20 na 21 ya Katiba ya JMT)
Kila mwanadamu unaemuona anaishi hapa Duniani bhasi jua kwamba ana mawazo yake tofauti na mwingine,ijapokuwa yanaweza kuwa mabaya ama mazuri lakini ndio mawazo aliyonayo kwa wakati huo uliopo. Katika kitu ambacho hakiwezi kuzuilika katika fikra za mwanadamu bhasi ni namna anavyofikiria kichwani mwake,ni kama siri nzito sana ambayo sio rahisi kwa mwanadamu mwingine kujua kile anachokiwaza mwenzake kwa nyakati hizo hata kama wakiwa ni mke na mume.
Sasa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake binafsi kuhusiana na jambo fulani katika nchi yetu ya Tanzania lakini pia mtu huyo huyo ana haki ya kupewa taarifa juu ya mambo yanayoendelea katika nchi hii. Pia mwananchi huyu ana haki ya kuchagua Imani aitakayo na kuiabudu lakini pia anayo haki ya kujishughulisha na mambo ya kijamii (shughuli za umma) pamoja na wananchi wenzake bila kuzuiliwa.
Kwa takribani miaka mitano iliyopita Tanzania yetu ilikumbwa na uvunjifu wa haki hii ya kikatiba ya watu kutoa maoni yao na kupewa taarifa stahiki wanazopaswa kuzipokea toka kwenye serikali yao. Kama ambavyo tumeona kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake binafsi kikatiba bhasi maoni hayo yanapaswa kusikilizwa hata kama yakiwa sio maoni ya kupendeza kwa maana ya kumfurahisha mtawala bhasi yaweze kuwa chachu ya kusukuma maendelo ya Taifa letu.
Uhuru huu wa utoaji maoni unaenda sambamba na wajibu wa kutoa maoni kwa kuzingatia lugha zenye staha kwa maana ya kujiepusha na lugha za matusi,kejeli,udhalilishaji na kutweza utu wa mtu. Mfano wa uvunjifu wa haki hii ni ile ya kutopewa taarifa rasmi za ugonjwa wa COVID19 pale ambapo kama Taifa tulihitaji kujua takwimu za ugonjwa na hata njia stahiki za kujilinda kama wananchi, hivyo kama mwananchi huyu anaweza kuwa na usawa baina yake na mwananchi mwenzake lakini pia endapo atakuwa amepata haki yake ya kuishi vile anavyostahili kwa mujibu wa sheria bhasi swala la kuwa na mawazo yeye fikra chanya kwa Taifa lake halitakuwa gumu na atakuwa mtu mwema asietegemea vyombo vya usalama kuja kumshurutisha kutii sheria.
HAKI YA KUFANYA KAZI (Inapatikana kwenye Ibara ya 22, 23 na 24 ya Katiba ya JMT)
Maandiko matakatifu ya Biblia (2 Wathesalonike 3:10) maneno ya Mtume Paulo yanasema “asiefanya kazi na asile” yalikuwa na maana ya kuwahimiza watu wafanye kazi ili waweze kujitegemea na hata katika maisha ya kawaida ukifanya kazi kwa bidii ndivyo utakavyokuwa na maendeleo yako binafsi ama familia yako pia. Kila mtanzania unaemuona leo hii bhasi jua kwamba ana haki zote za kufanya kazi hapa nchini katika nyanja zozote zile na pia ana haki ya kupokea ujira anaostahili kutokana na kazi hiyo anayoifanya ya kujiingizia kipato chake kama mwananchi wa Taifa hili.
Siku zote afanyae kazi bhasi baada ya malipo yake atajinunulia mali ama kumiliki mali kadha wa kadha na huko kumiliki mali hizo sio katazo la kisheria bhali ameruhusiwa kisheria kumiliki mali zake binafsi na endapo serikali itataka mali zake bhasi anapaswa kulipwa fidia juu ya mali zake alizozitafuta kwa jasho lake.
Swali chonganishi: Mnaikumbuka bomoa bomoa ya Kimara? Wale wananchi walilipwa fidia? Je ile bomoa bomoa ya kule Mwanza pia hali ilikuwaje?
Hivyo bhasi tunaona fika kwamba haki hizi za binadamu ni haki za msingi ambazo kwa mafikirio ya ustawi mzuri wa jamii yetu ya Tanzania zinapaswa kulindwa na kuenziwa vizuri ili tuweze kupeana changamoto zenye kuijenga nyumba yetu Tanzania iwe imara na Taifa lenye demokrasia nzuri kwasababu kama haki za binadamu zinaweza kuvunjwa hadharani bhasi haitakuwepo demokrasia ya kweli bhali uvunjifu wa amani na Katiba kwa ujumla wake. Nina hakika kwamba Taifa ambalo wananchi wake wanaishi kwa usawa,wana uhuru wa mawazo/maoni na wanafanya kazi zao pasipo kuzongwa zongwa na tozo za kodi zisizo na ulazima bhasi ni Taifa lenye ustawi mzuri na haliwezi kuwa Taifa tegemezi hata kidogo.
Maelezo: JMT - Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

- Haki ya usawa
- Haki ya kuishi
- Haki ya uhuru wa mawazo na
- Haki ya kufanya kazi

Upvote
1