Ufafanuzi kuhusu ajira UTUMISHI

Ufafanuzi kuhusu ajira UTUMISHI

lostone

Member
Joined
Jun 29, 2024
Posts
33
Reaction score
57
Habari za kazi kaka tunaomba utupazie sauti tuweze kufahamu sheria pamoja na utaratibu wa sekretarieti ya ajira utumishi katika mchakato wa usahili.

Hivi karibuni 1/09/2024 zilitangazwa ajira za kada ya afya kupitia sekretarieti ya ajira Baada ya mchakato wa kupata wanaostahili kwa usahili 27/08 kwajili ya usahili ambao ungepangwa kuanza tarehe 02/09/2024 wakianza kada ya afisa tabibu.

Lakini kuna kind kubwa la vijana walizuiliwa kuingia kwenyw chumba cha kufanya mitihani wakuandka kwa kigezo Cha kukosa kitambulisho chenye kuonesha leseni hai kutoka MCT kwa wakati huo huo ukiingia kwnye mfumo wa MCT kipengele Cha "search doctors " ukisachi jina la mtu huyo linaonesha yupo registered na legible to practice Yani amesajiliwa na anaruhusiwa kufanya kazi na hii huja Baada ya kuuhisha leseni kwa kulipia 75000 tsh kila mwaka.

Wakati huo huo Kuna kundi la watu wenye ambao hawakua na certificate of enrollment kutoka MCT waliruhusiwa kwa kutumia kigezo kwamba walikua na ID card ambayo inaonesha wako legible to practice sasa tunauliza Kama mfumo wa MCT anaonesha mtahiniwa yupo legible to practice wakati huo huo anakataliwa kuingia kwa mtihani kisa Hana ID kwa Karne ya Sasa ni kweli?
 
Zanzibar Kuna watu wameruhusiwa kufanya interview wakiwa hawana leseni ya MCT Wana leseni ya Zanzibar ambayo haitambuliwi na MCT eti wakimaliza interview wataifuatilia hiyo leseni hizi ni double standard.
 
Rais wa Tanzania kwa sasa anatokea Zanzibar.
 
Usaili umekua km movie,utumishi imekua kama polisi alafu graduates ndio wahalifu na wadanganyifu.km huna connection kutoboa bongo ni kazi
 
Zanzibar Kuna watu wameruhusiwa kufanya interview wakiwa hawana leseni ya MCT Wana leseni ya Zanzibar ambayo haitambuliwi na MCT eti wakimaliza interview wataifuatilia hiyo leseni hizi ni double standard.
Bara Kuna mtu kazuiliwa kisa barua ya utambulisho wa mkazi muhuri umefifia
 
Zanzibar Kuna watu wameruhusiwa kufanya interview wakiwa hawana leseni ya MCT Wana leseni ya Zanzibar ambayo haitambuliwi na MCT eti wakimaliza interview wataifuatilia hiyo leseni hizi ni double standard.
Na hizi ajira za bara wakazi wa znz wanaaply ila ikifika swala la kuaply kazi za znz wakazi wa Tanganyika inakua ngumu
 
Huwa kuna baadhi ya mambo watanzania ni wavivu kufuata utaratibu. Kama walisema uende na vitambulisho ABC wewe ukaenda huna B au C unategemea nini?
Utaanza kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu..

Sikatai kunachangamoto za kibinadam ila haiondoi wao kutofta utaratibu.

Tuache maisha ya mazoea katika mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom