Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
UFAFANUZI WA TAARIFA ILIYOCHAPISHWA KWENYE UKURASA WA JAMII FORUM TAREHE 17.03.2019 KUHUSU EWURA CCC
Tarehe 17.03.2019 kuna mdau ameandika taarifa inayolenga ama kwa kufahamu ama kwa kutokufahamu kupotosha umma wa watanzania kuhusu kazi na majukumu ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati ma Maji (EWURA CCC). Ufuatao ni ufafanuzi wa baadhi ya hoja alizoandika mdau huyo:-
1. EWURA CCC ni Taasisi inayojitegemea, na siyo kitengo ndani ya EWURA kama ilivyodaiwa na mdau aliyechapisha taarifa yake.
2. EWURA CCC imeundwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ya mwaka 2001, Sura ya 414 Kifungu cha 30. Lengo kuu ni kulinda na kuteteaa maslahi ya watumiaji wa huduma za nishati na maji zinazodhibitiwa na EWURA ambazo ni majisafi na usafi wa mazingira, umeme, gesi asili na bidhaa zitokanazo na petroli.
3. Majukumu ya EWURA CCC kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya EWURA Kifungu cha 31(1) ni kama yafuatayo:-
6. Utaratibu wa kulalamika unamtaka Mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake kwa maandishi kwa Mtoa huduma. Asipordhika na utatuzi, anapaswa kujaza fomu ya malalamiko ya EWURA na kuwasilisha malalamiko yake EWURA. Asiporidhika na utatuzi utakaofanywa na EWURA, mtumiaji anaweza kukata rufaa Baraza la Ushindani (FCT). Kwenye huo mchakato, jukumu la EWURA CCC ni kumsaidia Mtumiaji kuujua na kuufuata utaratibu huu ili lalamiko lake lipatiwe ufumbuzi.
7. Mathalan, kama mteja ana tatizo la umeme mdogo eneo lake, anachopaswa kufanya ni kutoa taarifa TANESCO kwani ndiyo taasisi yenye wajibu wa kuhakikisha umeme inaosambaza unakidhi viwango. Taarifa inapaswa kuwasilishwa kwa maandishi, na nakala abaki nayo mteja kwa ajili ya ufuatiliaji. TANESCO inawajibika kushughulikia kero iliyoripotiwa kwa mjibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO.
8. EWURA CCC inatoa rai kuwa, ni vyema wadau watumie muda wao kutafuta taarifa sahihi ili kuepuka upotoshaji usio wa lazima.
Huduma bora ni haki yako.
Imetolewa na EWURA CCC
17.03.2019
Pia, soma hapa >>> TBA na EWURA CCC kitengo cha walaji Zifumuliwe HARAKA au Zifutwe kabisa - JamiiForums

- Kufanya maamuzi, kutoa maoni/taarifa na kushauriana na EWURA, Wizara, Mawaziri wa sekta husika;
- Kupokea na kusambaza taarifa, maoni yenye maslahi kwa watumiaji;
- Kuanzisha Kamati za watumiaji za kimkoa na kisekta na kushauriana nazo;
- Kushauriana na Viwanda, Serikali Wadau wengine juu ya masuala yamhusuyo mtumiaji.
- Hivyo basi si kweli kwamba EWURA CCC ina Majaji kutoka Mahakama kuu kama ilivyosemwa na mtoa mada mtandaoni.
- Kazi ya kuhakiki ubora wa huduma siyo jukumu la EWURA CCC, bali la Mdhibiti (EWURA). Mamlaka nyingine yenye jukumu la kusimamia ubora wa huduma ni Shirika la Viwango (TBS).
- Kinachofanywa na EWURA CCC ni kuendelea kushauri/kuwakumbusha watoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa (service levels) na ambavyo kwa kawaida hujumuishwa kwenye mikataba ya huduma kwa wateja (client service charter).