Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

Unaonaje na wao waingizwe kwenye mifuko Hii, Kama kikokotoo Ni kizuri
Hawawezi kuwa pensionable sifa za kuwa pensionable ni Uchangie zaidi ya miaka 15 au Miezi 180, Mbunge anakaa madarakani miaka 5, Ajira anaajiriwa mtu ambaye yuko chini ya miaka 45 ili apate sifa za kuwa pensionable lakini Mbunge anagombea mtu mwenye umri hata juu ya 45. Kifupi wabunge hawawezi kuwepo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Utapewa mil 5 za bure za utetezi wa kikokotoo kipya kama Yale magoli ktk mechi za kimataifa
 
Lipeni fedha zao kwa mkupuo kama mnavyowalipa wabunge....Kama mtu amechangia zaidi ya miaka 15 basi apewe na pensioni yake ya kila mwezi ,mnatumia fedha zao kwenye miradi hewa na kutapakanya fedha kisha mnakuja na mipango ya kuwadhulumu wafanyakazi.
Ulicho kiandika ndicho kinacho fanyika.
 
Hakuna sehemu kwenye formula kuna 30 na 50.
Inaonekana umecopy hili bandiko mahali bila ata kupitia na kuelewa
Kikokotoo kipya cha:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 33%

Na kikokotoo cha zamani cha LAPF na PSPF yaani

1/540 × LAS x PoS x 15.5 x 50%
embu fafanua hizo inputs za mwisho 33% na 50%
 
Inaonekana umecopy hili bandiko mahali bila ata kupitia na kuelewa
Kikokotoo kipya cha:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 33%

Na kikokotoo cha zamani cha LAPF na PSPF yaani

1/540 × LAS x PoS x 15.5 x 50%
embu fafanua hizo inputs za mwisho 33% na 50%
1/580 : Kikokotoo Limbikizi
APE : wastani wa mishaara bora ya miaka mitatu, ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu
PoS : Miezi ya uchangiaji katika mfuko.
12.5 : Makadirio ya miaka 12.5 ya kuishi baada ya kustaafu
33% : Kiwango cha mkupuo

Mimi najibu ulicho andika kwenye swali lako uliweka Asilimia 50 na 30. Hii asilimia 30 uliyo andika mara ya kwanza uliitoa wapi...!?
 
Hujielewi wewe..na ulivyo sema hakuna 50% ulimaanisha nn?
 
Mkuu kuna hizi watu walikuwa ppf alafu wakahamishwa nssf kwa mashirika binafsi hivyo unakuta kule ppf walichangia zaidi ya hiyo miaka 15 alafu huku nssf anakama miaka minne alafu kulikuwa na deal ppf watu wakachukua hela yao yote wakabaki za nssf ila hawakupewa na riba swali langu ni je wakistaafu nssf watawalipa pension ya kila mwezi?
 
Kwa Mwanachama aliye changia mfuko zaidi ya Mmoja, ya NSSF na PSSSF.. Huyu akistaafu au kupatwa na janga lolote atalipwa na mifuko yote miwili kadri ya alivyo changia.

Kuhusu fao la uzee, atalipwa na mifuko yote miwili kwa kutumia Totalization formula, kote kote atapata KIINUA MGONGO na PENSHENI YA KILA MWEZI.
 
Kwa kikokotoo hiki ikitokea mnufaika anakufa ndani ya Mwaka mmoja inakuwaje kwa wategemezi wake?
 
Umetumwa wewe,unatumika.Mbona haujazungumzia uwekezaji usio na tija unaofanywa na mifuko.Mbona hujazungumzia ubadhirifu na ufisadi unaofanywa na mifuko.Hayo yote wa kuumia ni watumishi.
Come again.
 
Kinacho filisi mifuko ishindwe kutoa mafao mazuri sio kikokotoo; Sababu ni moja tu;
UENDESHAJI MBOVU KABISA WA MIFUKO HIYO NDIO UNAOIFILISI
Wana ajiri tu hovyo hovyo, hivi majuzi tulisikia sijui wameajiri watu 600 (in house) bila kutangaza, ina maana hapo wamejaza ndugu na marafiki; wameanzisha miradi ya Mabilioni yasiyo na tija yoyote na kwa gharama za kiupigaji; fuatilia magorofa waliojenga barabarani kule Arusha na miradi mingi tu ya hovyo hovyo
Jirani zetu Kenya wafanyakazi wanachangia kidogo kuliko wafanyakazi wa Tanzania ila wanasimamia mifuko Vizuri na kufanya uwekezaji wenye tija, mifuko yao ina Afya na hawana changamoto kama hizi za kwetu

Kwa kuona watu ni mambumbu ndio sababu wanashikilia kuwa tatizo ni kikokotoo kitu ambacho sio kweli !
 
Mfuko gani uli-ajiri watu 600 bila kutangaza...!?
 
Naunga mkono hoja. Ignorance is eating Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…