Ufafanuzi kuhusu speed High way

obinae

Member
Joined
Mar 10, 2018
Posts
32
Reaction score
19
Wakuu nahitaji ufafanuzi kidogo kuhusu hivi vibao vya speed barabarani.Mfano umeshamaliza kibao cha speed 50 baada ya hapo unatakiwa utembee na speed ngapi (Gari ndogo) maana mabasi najua yana ving'amuzi
 
Wakuu nahitaji ufafanuzi kidogo kuhusu hivi vibao vya speed barabarani.Mfano umeshamaliza kibao cha speed 50 baada ya hapo unatakiwa utembee na speed ngapi( Gari ndogo) maana mabasi najua yana ving'amuzi
Baada ya kibao cha 50 subiria mita 100 nyingine alafu baada ya hizo ni wewe, gari lako na Mungu wako. Cha ziada tu kama unataka kuovertake angalia kwa umakini side mirrors zako na mistari ya barabarani.

Cha ziada zaidi, ukiona kulia kwako kuna kibao kinachoruhusu magari ya nayoenda unakotoka yatembee zaidi ya 50, ujue fika hiyo eneo ni 50 hata kama hujabahatika kuona kibao.
 
Kuna siku nasimamishwa na trafiki barabaran ananiambia niko speed sana na kulikuwa hmna kibao cha speed 50 nami nilikuwa speed around 120 hvi,nilihic labda kuna maelekezo mapya siyajui
 
Kuna siku nasimamishwa na trafiki barabaran ananiambia niko speed sana na kulikuwa hmna kibao cha speed 50 nami nilikuwa speed around 120 hvi,nilihic labda kuna maelekezo mapya siyajui
Vipi mkuu, ulitoa hela ya kisusio???
mimi nilikua natoka dodoma naenda dar, mwanzoni mwanzoni tu kuna sehemu kulikua kuna bonde alafu kumenyooka.
Nikijiachia, nikasimamishwa na mmama. Akasema na makosa matatu, la kwanza mwendo wangu umechangamka, akangalia kwenye siti ya abiria akaona kuna risiti ya mafuta akafikiri ni risiti ya polisi na mie nikatembelea humo humo, akabaki mikono tupu.
Hadi leo sijui kosa la pili na la tatu, ingawa kwenye la kwanza pia sikuelewa
 
Kuna siku wamenisimamisha mmoja wao ananiambia kwamba nimesimamishwa kwa ajili ya spidi, nikamwambia, hii gari ina kikomo cha 240/ hr mimi nilikuwa 180/hr. Sasa inakuwaje unasema nimezidi speed ?. Kwa hasira akanifyatulia risiti na kunitupia dirishani, nilipandisha kioo na kuondoka kwa slip kali iliyowaachia vumbi la kutosha..!!

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Sikutoa maan nilikuwa na askari mwenzao kwenye gari akaingilia show tukaondoka....nikawa tu najiuliza haya mambo ya niko speed sana yanatokea wapi???
 
Khaaaaa eti mwendo umechangamka
 
Natumaini haikuwa kwenye kibao cha 50,kama ni hvyo sasa mtu unatakiwa kutembea na speed ipi baada ya kuvuta kibao cha speed 50??maana Hawa wazaa nguo nyeupe na zile kofia zao siwaelewi
 
Khaaaaa eti mwendo umechangamka
Hapa kwa kweli inabidi mtu aje atueleze, maana kuna wengine sie hatuwezi ubishani.
Na hawa watu ukionesha una uelewa usumbufu unakua mkubwa zaidi
 
Na mimi natamani niseme nilisimamishwa kwa mwendo kasi lakini bahati mbaya sina hata baiskeli [emoji24][emoji24][emoji24]
 
magari yote ya abiria na magari yote yenye kubeba uzito wa 3.5tons kwenda juu yaishie 80kph mahali ambapo hakuna speed limit.


magari yenye uwezo wa kubeba uzito wa 3ton kushuka chini yenyewe yatembea speed elekezi mahali ambapo kuna speed limit kwa mahali pasipo na speed limit basi madereva waendeshe speed yoyote ambayo ataweza kulimudu gari lake
 
Sasa kisimamishwa na kuambiwa mwendo wako umechangamka inakuaje???
Alafu hivi kuwasha taa wakati unatembea speed kubwa ni sheria ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…