Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikieleza malalamiko ya mdau kuhusu ukosefu wa dawa ya Trastuzumab kwa ajili ya matibabu ya saratani.
Hospitali inapenda kuufahamisha umma na wadau wote kuwa dawa ya Trastuzumab zinapatikana hospitalini hapo, kwa viwango vyote vinavyohitajika kimatibabu 600mg, 440mg na 150mg. Kulikuwepo na changamoto ya 440 mg kwa muda mfupi kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika lakini kwa sasa inapatikana.
Pia Hospitali ya Taifa Muhimbili ingependa kuwasisitiza wapata huduma wetu wote kufata taratibu za Hospitali za namna ya kupata majibu sahihi kwa changamoto zote wanazopitia wakati wa kupata matibabu, ili kuepuka kuwa na taarifa zisizo sahihi
Muhimbili inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu za matibabu ya saratani na magonjwa mengine, kwa lengo la kutoa huduma bora na za uhakika kwa wagonjwa wote.