Hospitali ya Taifa Muhimbili
Public Institution
- Apr 9, 2026
- 13
- 38
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu madai ya kutokuwepo kwa dawa ya Trastuzumab, inayotumika katika matibabu ya baadhi ya wagonjwa wa saratani.
MNH inapenda kuufahamisha umma, wagonjwa na wadau wote kuwa dawa ya Trastuzumab inapatikana hospitalini kwa nguvu zinazohitajika kulingana na mahitaji ya kitabibu, ambazo ni 600mg, 440mg na 150mg.
Pia soma ~ Mwezi wa pili sasa Mama amekosa Dawa ya Saratani (IV TRASTUZUMAB 440mg) Muhimbili Upanga
Ni kweli kwamba katika kipindi cha nyuma kulikuwa na upungufu wa nguvu ya 440mg kwa muda mfupi. Hata hivyo, nguvu nyingine za dawa hiyo zilikuwepo na ziliwezesha wagonjwa kuendelea kupata matibabu yao kwa kuzingatia miongozo ya tiba.
MNH inawataka wagonjwa na ndugu zao kutopata hofu kutokana na taarifa zisizothibitishwa zinazoweza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa changamoto au swali lolote linalohusu upatikanaji wa dawa na huduma za matibabu, wagonjwa wanashauriwa kutumia njia rasmi za mawasiliano za hospitali ili kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Hospitali ya Taifa Muhimbili inaendelea kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa dawa ikiwemo dawa zinazotumika katika matibabu ya saratani, kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma salama, bora na endelevu.
MNH inaendelea kuweka afya na ustawi wa wagonjwa wetu kuwa kipaumbele.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Huduma Bora kwa Afya ya Jamii