Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Watu wa Soka,
Juzi Jumanne 21/06/2022 saa 7:00 mchana tulimtambulisha rasmi mchezaji wetu mpya Habib Haji Kyombo ambaye tumemsajili kuja kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji.
Kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii (@singidabsfc) tulichapisha baadhi ya picha zake akiwa anasaini mkataba wa kuitumikia timu yetu kwa muda wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.
Hata hivyo, sintofahamu ikaibuka kwanini ameonekana na jezi za DTB FC badala ya Singida Big Stars?
Nimeona kipekee kabisa (exclusively) nifafanue mkanganyiko huo kupitia Jukwaa hili la JamiiForums kama ifuatavyo:
1. DTB FC ndiyo Singida Big Stars FC ya sasa. Taratibu zote za kisheria za kubadili jina zimeshakamilika na jina jipya linatumika kwenye mikataba na makubaliano yote ya kisheria ndani ya timu.
2. Habib Haji Kyombo tulimsaini mapema kabla hatujazalisha chapa/logo mpya ya Singida Big Stars pamoja na vifaa vingine kama jezi na kadhalika, hivyo kulazimika kumsaini akiwa na jezi yetu ya awali ya DTB FC.
3. Mkataba aliousaini Habib Haji Kyombo tayari ulikuwa na mabadiliko ya jina la timu, hivyo amesaini kama mchezaji wa Singida Big Stars FC na sio DTB FC.
4. Bado tunaruhusiwa kutumia chapa ya DTB katika kipindi hiki cha mpito (transition) kuelekea kubadilisha kila kitu kiwe Singida Big Stars FC.
5. Upo uwezekano jezi zitakapokamilika hivi karibuni, ataonekana kwenye picha nyingine akiwa na uzi mkali wa Singida Big Stars FC.
Asanteni sana.