Ufafanuzi mdogo kuhusu kauli ya mabadiliko ya kikokotoo

Ufafanuzi mdogo kuhusu kauli ya mabadiliko ya kikokotoo

DOMINGO THOMAS

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
365
Reaction score
365
Kabla ya kuanza kutumika kikokotoo cha asilimia 33% kwenye kiinua mgongo na asilimia 67% kwenye pensheni ya kila mwezi, kulikuwa na mifuko mitano (5) ambayo kila mmoja ulikuwa na formula yake kwenye ukokotoaji wa mafao ya uzee:

1. LAPF na PSPF: Asilimia 50% kwenye kiinua mgongo na asilimia 50% kwenye malipo ya kila mwezi (Monthly Pension).

2. PPF, NSSF na GEPF: Asilimia 25% kwenye kiinua mgongo na asilimia 75% kwenye malipo ya kila mwezi.

Kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba tarehe 13 Juni 2024:

1. Wanachama wa LAPF na PSPF: Watalipwa asilimia 40% kama kiinua mgongo (badala ya asilimia 33%), na malipo ya kila mwezi yatakuwa asilimia 60% (badala ya asilimia 67%).

2. Wanachama wa GEPF, NSSF na PPF: Watalipwa asilimia 35% kama kiinua mgongo (badala ya asilimia 33%), na malipo ya kila mwezi yatakuwa asilimia 65% (badala ya asilimia 67%).

3. Wanachama wa PPF, GEPF, PSPF na LAPF (PSSSF) kabla mifuko kuungana na baada ya kuungana waka-hamia NSSF, na walio kuwa NSSF kabla ya kuungana na waka-hamia PSSSF: Hawa wanatumia Totalization formula.

NOTED: Kauli hii bado haijaanza kufanya kazi mpaka pale miongozo na taratibu zitakapotolewa.

Imeandikwa na Thomas Ndipo Mwakibuja, Mtaalam wa hifadhi ya Jamii (Social Protection Expert).
 
Back
Top Bottom