habari MMU
tukiwa kwenye site hii pendwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na utani wa hapa na pale juu ya mapenzi n.k
me binafsi naona kuna mambo mawili
kwanza; kuna zile mada reeeefu mpaka hupelekea msomaji kufatilia comment za watu ili angalau kupata hata summary hivyo kusababisha mchangiaji kushindwa kuelewa dhamira ya mada hivyo atachangia kutokana na reply za wengine.
pili; kuna zile mada fupi tena ni za kueleweka hapo humfanya msomaji kuelewa haraka na kutoa mawazo yake sahihi na pia haimpotezei muda mwingi kufatilia mada moja tuu.
me binafsi napendelea mada fupi kwani hazichoshi.
vp we mdau wangu wa nguvu..?