Wadau wa JF kuna hili la usajili wa wanafunzi katika mfumo wa TCU
1. Hivi deadline ya kujisajili kwa form 6 waliomaliza 2015 ni lini? maana kwenye tangazo naona ile ya wale wa kurudi 2014
2. Na kiasi cha malipo ni kiasi gani maana dogo amenieleza ni 30,000 wakati kwenye tangazo naona 50,000? je kuna makosa sehemu?
Nauliza haya kwa sababu namba zao walizotoa kwenye tangazo zote tatu hazipatikani, sijui ni bahati mbaya au makusudi sijui!
mkuu soma hapo http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Call for Application form 6_2015.pdf itakusaidia kukuondolea ukungu na utata ulio nao