Ufafanuzi uliotolewa na uongozi wa Simba

Tusizunguke sanaa
Pesa ipo ama haipo? Kama imewekwa kiasi gani?.

Na kama bado je itawekwa lini?
Ni nini kinakwamisha mchakato huo mpka sasa?

Ndiyomana nikamwambia usome between the Line!

Makubali ya kuunganisha Kampuni (MO 49% na Simba SC 51%) hayafanywi na MO wala Simba bali ni lazima yasimamiwe na kukubaliwa na Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC).

Na kwahiyo MO haruhusiwi kuweka hata Cent 5 kama FCC hawajaridhia kuungana kwao, na iwapo ataweka basi FCC haitozitambua hizo hisa 49% za MO na Simba haitotambuliwa kama Kampuni bali itabaki kuwa Taasisi iliyosajiliwa na RITA kuwa inamilikiwa kwa 100% na Wanachama, hivyo MO hana chake.

KESI ILIYOPO:
Ni kutupiana mpira kati ya Simba Sports Club na FCC kila mmoja kumlaumu mwenzake kuwa ndiye anayekwamisha mchakato, Wala MO hahusiki na kukwamisha mchakato kwani yeye anayo Kampuni halali na kipengele cha kwake ni kuweka hela tu baada ya mchakato kutimia.

Sasa Simba Sports Club wao wanalaumiwa na FCC kukwamisha mchakato wa Mabadiliko kwa kutopeleka Documents Muhimu zinazotakiwa kama vile Audit ya mapato na matumizi ya miaka 5, thamani halisi ya mali za Simba na vielelezo vyengine ambavyo kiukweli Simba hawana.

Kwahiyo MO sasahivi sheria za FCC hazimruhusu kuweka hela kwani kuungana kwao bado hakujatambuliwa na FCC, akiweka tu hela hizo basi zitapigwa na isiwe lolote na MO hatakuwa na mamlaka ya kumiliki hisa 49% bali Simba Sports Club itabaki kuwa Taasisi inayomilikiwa na Wanachama kwa asilimia 100%.

Tatizo lenu washabiki wa Yanga munakomaa kiushabiki tu bila ya kujua kinachoendelea.
 
Poa sawa tumekubali
 
Sasa je hizi pesa anazotumia sasa zipo upande gani?
 
Sasa je hizi pesa anazotumia sasa zipo upande gani?

Sasahivi yeye ni Mdhamini tu kwahiyo hela anayotoa inahesabika ni Ruzuku wala haimo kwenye Mkataba wowote ule, likitokea lolote lile la Simba kuvunja udhamini wake basi hizo hela hawezi kurudishiwa wala hatopewa chochote cha kufidia hela aliyotoa!

Lakini mchakato wa mabadiliko ukikubaliwa tu na FCC basi MO akitoa 20B basi hizo hela zitabaki kuwa zake kwa thamani ya 49% na Simba wakitaka kuvunja Mkataba itabidi wazinunue hizo 49% kwa thamani ya 20B alizotoa au zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…