Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..

Ni kweli ocd Yuko chibi ya hao uliowataja. Lakini nadhani kama atazuia hiyo mikutano ya vyama vya siasa kwa kufuata maagizo kinyume na sheria anaweza kushitakiwa kama eye.
 
Ndugu, hii kesi ni ya kutengeneza ili hawa watawala waondoe kile wanachodhani kikwazo kwao kutawala kwa amani yaani CHADEMA/Freeman Mbowe tu...

But, their plan was poorly coordinated and therefore leading to poor implementation....

Sasa wamepoteana, hawaonani. Ni aibu tupu...!!

Ni bahati mbaya sana kuwa, baadhi ya mahakimu/majaji (MSISITIZO: sijasema wote, nimesema baadhi) wamekubali kushiriki mchezo huu hatari hata kuuchafua mhimili wote wa mahakama....!

Taabu ya Jaji Elinaza Luvanda kutoa maamuzi ya haki mbele ya sheria, yameathiriwa na msingi wa kesi yenyewe ambao ni UONGO WA MASHTAKA kiasi ambacho mwendesha mashtaka na Mawakili wa serikali wakashindwa kuutengeneza na kuutetea uongo wao na kumpelekea Jaji ambae naye ni sehemu ya plan hiyo haramu kuvurunda kujaribu kupindisha sheria machana kweupe bila haya...!!!

Na UONGO siku zote ni uongo tu. Huwa ni ngumu sana sana kujaribu kuupaka paka rangi ili ugeuke ukweli hususani kwenye maswala serious kama ya kudhulumu Uhuru, haki na uhai wa watu wengine...!
 

Once you have prejudged a matter it’s extremely hard to see the other side. Hata malaika wa Mungu akishuka kusikiliza hii kesi, kuna watu mtaukataa uamuzi wake, kama huo uamuzi ni wa kumtia Ayatollah Mbowe hatiani.
 
Ni kweli ocd Yuko chibi ya hao uliowataja. Lakini nadhani kama atazuia hiyo mikutano ya vyama vya siasa kwa kufuata maagizo kinyume na sheria anaweza kushitakiwa kama eye.
Kwani utendakazi wa jeshi lolote ni nini zaidi ya "amri na utekelezaji" ambavyo ndio hilo unalosema maagizo na maelekezo ambayo ni lazima atii.na wao wana uwanda mpana wa kukataa kwa sababu zao za kiintelijensia ambazo hawalazimiki kuzisema hadharani.so mkutano wa pamoja na viongozi wa juu ni muhimu na nashauri wapinzani wasisuse,kwani hawatapata suluhu
 
Mkuu zipo nyingi tu, nenda Tanzlii alafu search 'Oxygen principle/Overriding principle' zitakua kesi zakutosha uzisome vizuri utaelewa Mkuu, ukiweka hisia pembeni tapata majibu ya maswali mengi sana Mkuu, tatizo umeweka sana hisia mbele hata hautaki 'ku-reason' Mkuu.

kusema Mh. Mbowe tu ndio mwenye haki hii kesi ni kukosea Mkuu, amhuri inayo haki ya kushitaki kwa niaba ya wananchi hiyo ni kazi na haki yake, sasa tatizo wewe umeikataa kabisa (sijui kama unajua hili au haujui).

Tumia 'case laws' ndio utaelewa hiyo principle ya kutokuamua kesi kwa kuangalia technicalities Mkuu. Sheria ni pamoa na kesi zilizoamuliwa na Mahakama Kuu/Mahakama ya Rufaa, kwa maana hiyo usishangae kwanini nimekuambia usome kesi kupitia Tanzlii Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…