Ufafanuzi wa Mapigo Kumi ya Wamisri!

ChamaDola

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
3,431
Reaction score
2,804
SEHEMU YA KWANZA
Lengo kuu zaidi la Mungu
lilikuwa ni kuwatoa Wamisri toka
katika Utumwa wa Kifkra na Kiimani wa
kuamini miungu mfu
iliyowapotezea muda na mali,vitu ambavyo
wangeweza kuvitumia kumjua
Mungu wa Kweli badala ya
kupoteza muda kuabudu miungu
isiyo na uhai na yenye kuishi tu kwenye
fikra za Wamisri!
Japo kisayansi na kiteknolojia walikuwa mbali,ila kiimani na kidini walikuwa maututi!

Ndiyo kusema,hii Miungu haikuishi
popote,zaidi kwenye fikra za
Wamisri!
Na mapigo haya yalilengwa
kuwaonesha Wamisri kuwa
miungu walioiumba wenyewe kifkra
haikufaa iwatishe!
Mungu alitaka kuwaonyesha
kuwa,Yeye mwenye kwa Mkono
mmoja anaweza kupambana na
Miungu yao yote kwa mamia
yake na akaitoa knockout!
PIGO LA KWANZA
Mto Naili ulikuwa ndiyo uti wa
mgongo wa Uchumi wa Misri kwani
uliwapa:Maji katikati ya
jangwa,samaki ,na magugu maji
kwa ajili ya kutengenezea nguo
na karatasi za kuandikia(papyrus
reeds)!
Mungu alipoyageuza maji kuwa
damu,ndani ya fikra za Wamisri
yoyote ni kuwa mungu wao wa
Mto Naili:HAPI,alishindwa kazi!
Kama HAPI,alishindwa jambo
dogo la kucontrol maji,je
atayaweza maisha ya watu?
Mungu 1-0 Miungu Makinikia!
PIGO LA PILI
Baada ya uvundo wa damu
kuwatesa kwa wiki moja,Mungu
akawaleta vyura toka mto Naili!
Chura hawa walisambaa Misri
nzima kasoro kule Gosheni!
HEKET,ndiye alikuwa mungu
mwenye kichwa cha chura,na
ndiye aliyehusika kuwacontrol!
Sasa,kama aliwashindwa
chura,ataweza kuwapa uzazi
wanawake na kuwapa maisha
marefu Wamisri?
Maana alikuwa pia mungu wa
uzazi na maisha!
Mungu 2-0 Miungu Makinikia!
PIGO LA TATU
Baada ya HEKET kuwashindwa
vyura,ikawa zamu chawa!
Baada ya Aaron kuipigiza fimbo
yake ardhini,vumbi lote la Misri
likageuka Chawa!
KHEPRI,alikuwa ni muumbaji,cha
ajabu alishindwa kuumba chawa
mavumbini,basi kama alishindwa
kuwaumba,je kuwarudisha
mavumbini!
TROTH,alikuwa ni mungu wa
miujiza,japo aliwasaidia wachawi
wa Farao kuiga mapigo mawili
ya mwanzo,ila hapa waligonga
mwamba!
Hata wale wachawi wawili
Jannes na Jambres( 2 Timotheo
3:8-9) walikiri mziki mnene!
PIGO LA NNE
Nzi ndiyo lilikuwa pigo nne!
Waliingia katika kila tundu la
mwili!
Kama HEKET aliwashindwa
chawa,basi KHEPRI aliwashindwa
nzi!
KHEPRI alikuwa na kichwa cha
mdudu,na nzi kuwatesa
watu,ilimanisha hana uwezo wa
kuwacontrol wadudu!
Sasa,kama kawashindwa
wadudu,atawaweza watu?
PIGO LA TANO
Mifugo yote ilikuwa ndiyo ya tatu
ya Uchumi wa Misri ukiacha
nguzo zingine mbili:Watumwa na
Mto Naili!
Wanyama hawa walikuwa ni
chanzo cha Chakula,walifanya
kazi ya shamba,walibeba mizigo
na watu!
Miungu iliyohusika na
mifugo,ilionekana si lolote wala
chochote!
1)HATHOR-mungu mke mwenye
kichwa chenye pembe za
ng'ombe,alipigwa kikumbo!
2)RA-mungu ne mwenye umbo la
maksai,naye alichezea za
chembe!
Sasa,kama miungu hii ilishindwa
kuilinda mifugo ya
Wamisri,ingeweza kulinda
maisha yao?
 
Pendael24 hapana, Kila pigo la Mungu wa Waisraeli lililenga kumuharibu mungu mmoja wa Misri!
Kihistoria,mapigo haya bado yana nadharia nyingi,kuna wingine wanasema yaliwahi kutokea na kuna wengine wanadai ni hadithi tu kama za sungura na fisi!
 
Haya mapigo kumi yana nadharia mbalimbali. Kuna nadhalia moja, ambayo na mimi naiamini sana inasema kama ifuatavyo:
  1. PIGO LA NILE KUWA DAMU: Mto naili hutiririsha maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia na sudani. Huko unakoanzia kuna nchi yenye udongo mwekundu. Ilitokea mvua kubwe ilinyesha, udongo mwekundu ukasombwa na hatimae mto nile kuwa mwekundu sababu ya udongo. maji ya nili hayakugeuka damu, bali lilikuwa tope jekundu.
  2. PIGO LA VYURA: Baada ya mto nili kujaa tope jekundu, vyura wake (mtoni) walishindwa kuishi katika hali ile na iliwalazimu kutoka nje ya mto, hivyo kulandalanda katika nchi ya misri wakitafuta maji safi kwa ajili ya kuzaliana, ikizingatiwa kipindi cha maji mengi ndipo vyura huzaliana.
  3. PIGO LA NZI: Wale vyura waliokimbia mtoni na kurandaranda nchi kavu waliishia kufa kwa sababu ya kutozoea mazingira. hivyo inzi wakapata ahueni ya kuzaliana kwa sababu ya uchafu uliosababishwa na kufa kwa vyura hao.
  4. MARADHI: Kuenea kwa maiti/mizoga ya vyura, harufu mbaya na kuzagaa kwa mainzi kulisababisha nchi kukumbwa na maradhi ya mlipuko, ukiwemo ugonjwa wa majipu.
  5. NYOKA.: Hawa viumbe walienea nchini wakisaka vyura. vyura walipotoweka mitoni iliwalazimu nyoka kutafuta vyura wengine au chakula kingine popote kilipo.
  6. VIFO; hivi vilitokea sababu ya maradhi kama iliyoainishwa hapo juu, pamoja na kukosekana ka maji safi ya kunywa.
 
Toka lini chura akakimbia maji yenye vumbi!!!!!

Halafu,mbona chawa hujawaandikia nadharia yao???
 
Toka lini chura akakimbia maji yenye vumbi!!!!!

Halafu,mbona chawa hujawaandikia nadharia yao???
Maji ya mto nili yaligeuka tope, sababu ya mvua kubwa iliyonyesha nyanda za juu. Chura si mvumilivu kwenye tope, hasa akitaka kuzaliana.
Nikuchekeshe kidogo? Chawa waliibuka baada ya wamisri kuishi siku nyingi bila kuoga wala kusafisha mavazi yao, baada ya kukosa maji safi.
 
Sawa tunakubaliana na fikra zako, LAKINI ni kwanini Firauni alikubali kuwaruhusu watumwa wale kuondoka? Vipi kuhusu bahari kuachia njia ili watumwa wale wapite kisha kujifunga pindi askari wa Firauni walipoingia katika bahari ile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…