ChamaDola
JF-Expert Member
- Dec 23, 2016
- 3,431
- 2,804
Wakuu,
Baada ya kuyaangalia mapigo
matano ya kwanza,ebu tumalizie
matano mengine!
Baada ya wanyama wa mwituni
na nyumbani kufa,pigo la sita
lilifuatia!
PIGO LA SITA
Musa aliyachota majivu ya jikoni
na kisha kuyarusha hewani!
Majivu hayo yakawa kama
kirusi,kwani kila yaliyomgusa
alipata vidonda mfano wa jipu
lenye kutoa majimaji,huku
yakiuma sana!
Hayakuchagua,maskini na hata
Farao yalimsomesha namba!
Lengo la Mungu lilikuwa
kuwafumbua macho
Wamisri,kuwa miungu yao
haikuwa na uwezo wowote!Kwa
Wamisri kuugua vidonda,hii
ilimanisha kuwa miungu yao
lishindwa kazi!Pigo hili
halikuiacha miungu ifuatayo
salama:
a)ISIS-huyu alikuwa ni mungu
mke aliyejishughulisha na
utabibu wa magonjwa ya
mlipuko!
b)SEKHMET-huyu alikuwa mungu
mme mwenye kichwa cha simba
aliyejihusisha na kuzuia
tauni,magonjwa na mabalaa!
Kama wakubwa walishindwa
kwa wingi wao na Mungu
mmoja,je maisha ya Wamisri
yako salama?
PIGO LA SABA
Baada ya siku kadhaa ya onyo
kuwa kuna mvua ya mawe
itashuka juu ya Misri yote,mawe
makubwakubwa yalianza
kuanguka!
Anga lilikunya mawe ya
haja,ambayo yaliua na kuharibu
miundombinu na mali!Na kama
haitoshi mvua hii ilinyesha
kipindi cha mavuno ya ngano na
shairi!Mavuno haya ndiyo uti wa
mgongo uliokuwa umebaki!
Uchumi wa Misri ulikuwa
unachechemea,kwa pigo hili
uchumi ulikufa kibudu!Miungu ya
Wamisri ilikuwa wapi kuzuia
tafrani hii?
A)NUT-mungu mke wa anga
aliyeuleta usiku na mchana!
Wamisri walijiuliza,je mama huyu
amepitiwa na usingizi?mbona
ameshindwa kulifunga anga
lake,ili lisivuje?
B)SHU-mungu mme wa hewa
C)TEFNUT-mungu mke wa maji na
unyevuunyevu!
Hawa miungu ofisi yao ilikuwa
anga,je walishindwa kuizuia
anga lisivuje mpaka balaa
likawanyea Wamisri!?
PIGO LA NANE
Miti michache iliyobakia
ilimalizwa na nzige walioijaza
Misri yote!Wamisri waliliangalia
anga huku wakimuuliza mungu
wao SENEHEM,Whatsup?what is
going on up there?
Huyu ndiye aliyehusika na kuzuia
magonjwa ya mimea na
wanyama!
PIGO LA TISA
Kama unafikiri giza la TANESCO ni
shida basi umejidanganya!Giza
hili liliifunika nchi yote kwa siku
tatu mfululizo!
Ilibidi kupapasa ili kujua
unaeoda wapi?Miungu ya
Wamisri ilienda wapi?Miungu hii
ilikuwa jipu:
A)RA-mungu mme
aliyeshughulika na mawio na
machweo ya jua!
B)HORUS-mungu mme aliyekuwa
na macho mawili:jua na mwezi!
Ilikuwaje macho yake
yakashindwa kuona na kuangaza
mchana na usiku?Kama hawa
majabali wawili walishindwa
kuiangaza dunia,je wataweza
kuiangaza mioyo ya Wamisri?
PIGO LA KUMI
Pigo hili lilifunga mahesabu!
Mzaliwa wa kwanza wa
mnyama,Mmisri na Farao wote
walikufa!
Farao alipoteza mrithi wa kiti cha
Ufalme wake na kupelekea
kuwaruhusu Waisraeli
kuondoka!
Miungu ya Wamisri ilichakazwa
na mkono wa Mungu mmoja!
Na Mungu huyu aliichapa miungu
yao katika uwanja wa nyumbani!
Baada ya kuyaangalia mapigo
matano ya kwanza,ebu tumalizie
matano mengine!
Baada ya wanyama wa mwituni
na nyumbani kufa,pigo la sita
lilifuatia!
PIGO LA SITA
Musa aliyachota majivu ya jikoni
na kisha kuyarusha hewani!
Majivu hayo yakawa kama
kirusi,kwani kila yaliyomgusa
alipata vidonda mfano wa jipu
lenye kutoa majimaji,huku
yakiuma sana!
Hayakuchagua,maskini na hata
Farao yalimsomesha namba!
Lengo la Mungu lilikuwa
kuwafumbua macho
Wamisri,kuwa miungu yao
haikuwa na uwezo wowote!Kwa
Wamisri kuugua vidonda,hii
ilimanisha kuwa miungu yao
lishindwa kazi!Pigo hili
halikuiacha miungu ifuatayo
salama:
a)ISIS-huyu alikuwa ni mungu
mke aliyejishughulisha na
utabibu wa magonjwa ya
mlipuko!
b)SEKHMET-huyu alikuwa mungu
mme mwenye kichwa cha simba
aliyejihusisha na kuzuia
tauni,magonjwa na mabalaa!
Kama wakubwa walishindwa
kwa wingi wao na Mungu
mmoja,je maisha ya Wamisri
yako salama?
PIGO LA SABA
Baada ya siku kadhaa ya onyo
kuwa kuna mvua ya mawe
itashuka juu ya Misri yote,mawe
makubwakubwa yalianza
kuanguka!
Anga lilikunya mawe ya
haja,ambayo yaliua na kuharibu
miundombinu na mali!Na kama
haitoshi mvua hii ilinyesha
kipindi cha mavuno ya ngano na
shairi!Mavuno haya ndiyo uti wa
mgongo uliokuwa umebaki!
Uchumi wa Misri ulikuwa
unachechemea,kwa pigo hili
uchumi ulikufa kibudu!Miungu ya
Wamisri ilikuwa wapi kuzuia
tafrani hii?
A)NUT-mungu mke wa anga
aliyeuleta usiku na mchana!
Wamisri walijiuliza,je mama huyu
amepitiwa na usingizi?mbona
ameshindwa kulifunga anga
lake,ili lisivuje?
B)SHU-mungu mme wa hewa
C)TEFNUT-mungu mke wa maji na
unyevuunyevu!
Hawa miungu ofisi yao ilikuwa
anga,je walishindwa kuizuia
anga lisivuje mpaka balaa
likawanyea Wamisri!?
PIGO LA NANE
Miti michache iliyobakia
ilimalizwa na nzige walioijaza
Misri yote!Wamisri waliliangalia
anga huku wakimuuliza mungu
wao SENEHEM,Whatsup?what is
going on up there?
Huyu ndiye aliyehusika na kuzuia
magonjwa ya mimea na
wanyama!
PIGO LA TISA
Kama unafikiri giza la TANESCO ni
shida basi umejidanganya!Giza
hili liliifunika nchi yote kwa siku
tatu mfululizo!
Ilibidi kupapasa ili kujua
unaeoda wapi?Miungu ya
Wamisri ilienda wapi?Miungu hii
ilikuwa jipu:
A)RA-mungu mme
aliyeshughulika na mawio na
machweo ya jua!
B)HORUS-mungu mme aliyekuwa
na macho mawili:jua na mwezi!
Ilikuwaje macho yake
yakashindwa kuona na kuangaza
mchana na usiku?Kama hawa
majabali wawili walishindwa
kuiangaza dunia,je wataweza
kuiangaza mioyo ya Wamisri?
PIGO LA KUMI
Pigo hili lilifunga mahesabu!
Mzaliwa wa kwanza wa
mnyama,Mmisri na Farao wote
walikufa!
Farao alipoteza mrithi wa kiti cha
Ufalme wake na kupelekea
kuwaruhusu Waisraeli
kuondoka!
Miungu ya Wamisri ilichakazwa
na mkono wa Mungu mmoja!
Na Mungu huyu aliichapa miungu
yao katika uwanja wa nyumbani!