Ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya wadau wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne-2013

Dah hawa NECTA bhaanaa hataree"
Watwabwie sasa kuingia A_Level wanachukua vigezo gan
 
History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz

HGK inakuhusu
 
Kwamba ufafanuz wa wapi watachaguliwa kuendeleana ngaz za juu utatolewa,hii inanipa wasiwas kwamba inawezekan hakuna mipango iliyo kamili mpaka watakapo kaa na kujadi n wap watawapeleka,kama upo kwann bas usitolewe mapema ili watu wajue mbiv na mbich my take balaza wafanye kaz zao kwa weledi kwa kuzingatia maslah ya nchi na sio matakwa binafsi au makundi flan hasa ya kisiasa
 
Kwa hyo mwenye E flat ni sawa na aliyepata F? Hawapati vyeti?
 


Inasemekana wamebadilisha mawazo wakafanya tofauti na ilivyopangwa awali:
"Kwa mfumo huu, alama ya ufaulu ilikuwa iwe E na CA zilitakiwa kuchangia asilimia 40. Hata hivyo mfumo huo haukutumika kama ilivyotangazwa na badala yake alama ya ufaulu imekuwa D na CA zimechangia 30, jambo ambalo bado halijawafurahisha wadau."
(SOURCE: Mwananachi)
 
Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi. Ika nimezidi kuchanganyikiwa, unaposema wamebadilisha mawazo hao ni akina nani? Kumbuka kuwa Prof Mchome alipokuwa anatangaza viwango vya ufaulu alisema kuwa vimetokana na mawazo ya wadau. Sasa inawezekana kweli jambo ambalo lilitokana na mawazo ya wengi kupitia madodoso libadilishwe tu eti kwa sababu WAMEAMUA KUBADILISHA MAWAZO? HAO NI AKINA NANI TUWAJUE? NCHI INAONGOZWAJE NDUGU ZANGU YAANI MTU ANAWEZA AKAAMKA AKAJIAMULIA TU JAMBO LINALOATHIRI WATANZANIA KADRI ANAVYOTAKA YEYE?
 
Mkuu Cambri,
Uchaguzi wangu wa maneno ("kubadili mawazo") haukuwa mzuri.
Kinachoonekana ni kwamba mipango ya awali imebadilishwa kama inavyosomeka kwenye quote niliyoweka hapo toka Mwananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…