Ufafanuzi: Waziri Ummy asema Shule Shikizi zipo nchini, hutokana na kuhamahama kwa wakulima ama wafugaji

Ufafanuzi: Waziri Ummy asema Shule Shikizi zipo nchini, hutokana na kuhamahama kwa wakulima ama wafugaji

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Waziri TAMISEMI, Ummy Mwalimu ametolea ufafanuzi kuhusu video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha wanafunzi wa madarasa tofauti wakitumia chumba kimoja cha darasa huku walimu wakiendelea kufundisha.



Waziri Ummy amesema haya...

Hii kweli inafadhaisha, Hizi tunaziita satellite schools ambazo vinajitokeza kutokana na kuhamahama kwa wakulima ama wafugaji. Huacha vijiji vyao na kuanzisha makazi mapya. After 3 years watoto wanakuwa na hivyo kuhitaji shule. Ndio wanaanzisha shule kama hizi.

Na wanatafuta wao wenyewe walimu wao. Na mara nyingi hawaripoti kuanza kwa shule hiyo Serikalini. Baadae wakiona wamezidiwa ndio wanatafuta namna ya kusaidiwa. Anyhow.

Uongozi wa Mkoa wa Iringa unalifuatilia na kuona namna bora ya kutatua changamoto hii.

Shule hii haijasajiliwa. Na zipo maeneo mengi nchini. Mwezi July 2021 tumeanza utaratibu wa kuzibainisha shule zote ambazo sio rasmi ili kuweza kuwaunga mkono wananchi kwa kujenga madarasa mengine na kupeleka walimu ili watoto hawa wapate haki yao ya elimu bora.

----
Satellite School kwa mujibu wa UNESCO

20210805_002210.jpg
 
Hii kweli inafadhaisha, Hizi tunaziita satellite schools ambazo vinajitokeza kutokana na kuhamahama kwa wakulima ama wafugaji. Huacha vijiji vyao na kuanzisha makazi mapya. After 3 years watoto wanakuwa na hivyo kuhitaji shule. Ndio wanaanzisha shule kama hizi.

View attachment 1880311
Wanapoelekea watatwambia habari za kuzaliwa kwa dish schools,kiufupi tutaelewana tu hamna namna.
 
Inaweza kuwa ni sahihi.. Na ndio maana hiyo shule ukimsikiliza mwalimu inaishia darasa la tatu, kwamba ni mpya.

Kuna mwaka nilienda Namtumbo, kuna misitu wasukuma wamehamia huko wanafuga na wako mbali na makazi ya watu. Hao lazima mbeleni nao waanzishe shule kama hii kwa maana watendaji wa vijiji huwalazimisha kupeleka watoto shule ukifika umri wa kwenda shule.
 
Sioni ubaya wa hizo shule, hasa kama wao hutafuta walimu wao na wakajiridhisha na viwango vyao, muhimu hapo wapewe msaada hitajika na serikali ikibidi hizo shule ziwe za kudumu kabisa ziendelee mpaka darasa la saba, kwani hii nchi bado tunaona ina upungufu wa vyumba vya madarasa hadi maeneo ya mijini.
 
Nimeshawai fanya kazi na UNICEF tulikuwa tuna deal na hizi shule ambazo ni satellite.

Nilipoona mapovu ya watu nikawa nacheka tu najisemea hawa hawaijui hata Tanzania.
 
Wanafunzi wanapata wakati mgumu sana hapo.

Nalog off
 
Wananchi wanahama hama kwa kutafuta maji kwaajili ya mifugo yao. Vijiji vingekua na maji tiririka ya uhakika wafugaji wangetulia na kuendeleza kilimo sambamba na ufugaji wao.
 
Back
Top Bottom