Nsennah
JF-Expert Member
- Jan 9, 2021
- 1,947
- 1,554
Wadau, picha yajieleza hapo!! Hofu yangu ni moja na pengine watanzania naomba mnifafanulie. Kukiwa na punguzo la bei ya mafuta ya petroli sokoni bei isishuke bali ibaki kama hapo awali? Kwa tafsri hiyo ni kwamba sheria ikiwekwa kama bei ni 3000tsh kwa lita hata ikishuka sokoni na kustahili kuwa 2970 bado ibaki 3000 na pesa iliyotakiwa kupunguzwa (30tsh) ndo ielekezwe kwenye mfuko wa barabara?
Na ikipanda sokoni ikawa 3200tsh itamuathiri mlaji atalazimika kununua kwa 3200 na endapo itashuka kwenye soko na kuwa 3100tsh, bei itaendelea kuwa 3200 hiyo 100 inaelekezwa kwenye mfuko wa barabara?
Napenda kufahamu zaidi kwenye hili maana naliona kwa upande wa mtumiaji wa mwisho kuendelea kuwekewa bei isiyo rafiki kwa mlaji wa mwisho kutofaidika na price fluctuation ya petroli.
Nawasilisha kwa ajili ya ufahamu zaidi.
Pia soma:Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wamefikiwa, wawekewa tozo ya 382 kwa kila kilo