Ufahamu mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa Faida Fund

lui03152

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2020
Posts
266
Reaction score
377
Wana JF,

Ninaomba mniambie, kwa watu waliowahi kuwekeza wanapata manufaa gani. Je, huu mfuko ni sawa na kununua hisa?

Je, unapataje manufaa? Mwanye uzoefu anieleze tafadhali, asante.
 
Wanajanvi, ninaomba mniambie, kwa watu waliowahi kuwekeza wanapata manufaa gani. Je huu mfuko ni sawa na kununua hisa? Je unapataje manufaa? Mwanye uzoefu anieleze tafadhali, asante.

Kaka tafuta nyuz za UTT zimejaa sana humu. Anyway kwa kifupi unit trust funds sio sawa na hisa za kawaida kwa maneno machache ni hivi

Kama unanunua hisa za kawaida utanunua hisa za kampuni husika direct au kama ni Bonds za Govt utanunua direct.

Ukiwekeza kwenye trust funds .. Fund manager anaichukua ile pesa yako anaigawa nyingine atawekeza kwenye hisa nyingine bonds.. ila kwa kesi ya Bonds 90% itawekezwa kwenye Bonds

Faida ya Trust funds ni kuwa unaweza kuwekeza kuanzia kias kidogo. Hata 5000 tu... sababu fund manager anakusanya pesa kwa watu wengi tofaut tofauti na kama ukiamua kuwekeze direct kwenye Bonds maana yake unatakiwa uwe na kias kikubwa cha pesa

Bonds ina low risk na interest ni kati ya 9% hadi 12% inategemea na mwaka husika.. pia ukiwekeza chini ya 5m utapata gawio mara mbili kwa mwaka na juu ya 5m utapata gawio kila mwez...
 
Like it
 
Nashukuru sana mtaalam...
 
Lakini kauliza kuhusu FAIDA FUND na sio hiyo uliyoelezea UTT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Faida fund mfuko mpya wa watumishi investment? Kama nihuo sidhani kama watu wanaujua vizuri maana ni mfuko mpya huo
 
Lakini kauliza kuhusu FAIDA FUND na sio hiyo uliyoelezea UTT

Sent using Jamii Forums mobile app
oh yes nili overlook ila FAIDA FUND na UTT zote ni TRUST FUND.. tofauti FAIDA SASA INA MFUKO MMOJA ni kama vile walivyoanza UTT na Mfuko mmoja.. so FAIDA FUND NI kama mfuko wa wekeza Maisha wa UTT.. unafanana kila kitu.. na hawana magawio ya mwezi faida yako inakuwa conveted kwenye vipande.. kwa kifupi faida yako inakuza mtaji.. ukitaka pesa unaenda kuuza vipande vyenye thaman unayotaka
 
Nashukuru sana mkuu hapa nimepeta kitu
 
Sasa ipi nzuri kwa mtu mwenye malengo ya muda mrefu
 
Sasa ipi nzuri kwa mtu mwenye malengo ya muda mrefu
Yote inafafana bosi tofauti waendeshaji... ila UTT ni mfuko wa zamani umeshaji establish FAIDA fund ni mpya hata mwaka hauna.. so ukiniuliza upi unafaa ofcourse nitakwambia UTT sababu tayari unamatokeo yanayoonekana

nitakupa njia rahisi ya ww mwenyewe kufanya maamuzi

ingia kwenye website zao zote zinamaelezo ya kutosha na bei za vipande ila UTT unaweza pata bei ya kipande toka kila mfuko ilipoanzishwa so chukua bei ya kipande ya mfuko unaotaka toka ulipoanzishwa mathalani huo mfuko wa wekeza maisha landa ulianzishwa 2004.. au ukwasi kisha angalia na bei ya sasa labda bei ya leo..

hii itakupa picha mfuko umekuwa ukipanda thaman kwa kiasi gani... labda shilingi 5 au 10 au hata 30 kila mwezi maana yake utapiga hesabu ungekuwa umejiunga na mfuko huo 5 au 10 years ago mpaka sasa hivi pesa yako ingekuwa imekuwa kwa kiasi gani...

FAIDA fund ndo mameanza so hawana data za kutosha pengine wana data za mie 6 nyuma maana yake.. ukilinganisha na UTT wana data za zaidi ya 10 years kwa hiyo utaona kuwa at least kwa UTT unaweza pata picha mifuko yao thaman zinavyopanda na kushuka na hii itakuwezesha kujua mfuko upi unafaa kwa malengo yapi.. kwa FAIDA fund inabidi uende kwa imani kuwa kwa trend ya kukua ya shilingi 3 kwa mwez basi ikiwa constant basi walau ndani ya miaka kadhaa nina kias flani. na wana mfuko mmoja tu.
 
Shukrani mkuu nimepata kitu si haba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…