Misitu na Nyuki
Member
- Mar 6, 2019
- 42
- 23
Leucaena leucocephala
Ni mti unaosaidia kusahihisha ama kurudisha Naitrojeni katika udongo, lakini pia ni mti unaokua haraka zaidi na asili yakeni Amerika ya kusini pamoja na Mexico.
Majani ya huu mti yakiwa mateke teke yaani hayajakomaa ni mboga nzuri na yana virutubisho vingi sana ambavyo ni muhimu kwa mwili.
Pia una sifa nzuri kwa ajili ya kuvuna mbao kutengeneza malighafi za ujenzi, kuaandaa kuni na pia kutumika katika kutengeneza karatasi viwandani.
Lakini pia mti huu ni mzuri zaidi katika kilimo mseto zaidi ni pale ukipanda miti aina hii ndani ya shamba la mazao kama mahindi, kwa sababu unasaidia na kurahisisha upatikanaji wa Naitrojeni ambayo ni muhimu kwa mazao ili kuweza kukua vizuri zaidi na kuongeza uzalishaji ama mavuno yako.
Kwa wafugaji nyuki huu mti ni muhimu sana kwani hutoa maua mazuri karibu ndani ya mwaka wote hivyokupelekea mazao ya nyuki kuwa mengi kwani hakula cha nyuki na maua mazuri.
Mlusina hufananishwa na mkunde mwingine (alfaalfa) muhimu kwa wingi wa virutubisho haswa protini kwa ajili ya mifugo. Lakini Mlusina una upungufu wa sodium na iodine lakini una wingi wa b -carotene.
#HifadhiMitiKwaFaidaYaTaifa