Ufahamu Mti wa Mlusina (Leucaena leucocephaela)

Joined
Mar 6, 2019
Posts
42
Reaction score
23
Leucaena leucocephala


Ni mti unaosaidia kusahihisha ama kurudisha Naitrojeni katika udongo, lakini pia ni mti unaokua haraka zaidi na asili yakeni Amerika ya kusini pamoja na Mexico.

Majani ya huu mti yakiwa mateke teke yaani hayajakomaa ni mboga nzuri na yana virutubisho vingi sana ambavyo ni muhimu kwa mwili.

Pia una sifa nzuri kwa ajili ya kuvuna mbao kutengeneza malighafi za ujenzi, kuaandaa kuni na pia kutumika katika kutengeneza karatasi viwandani.

Lakini pia mti huu ni mzuri zaidi katika kilimo mseto zaidi ni pale ukipanda miti aina hii ndani ya shamba la mazao kama mahindi, kwa sababu unasaidia na kurahisisha upatikanaji wa Naitrojeni ambayo ni muhimu kwa mazao ili kuweza kukua vizuri zaidi na kuongeza uzalishaji ama mavuno yako.

Kwa wafugaji nyuki huu mti ni muhimu sana kwani hutoa maua mazuri karibu ndani ya mwaka wote hivyokupelekea mazao ya nyuki kuwa mengi kwani hakula cha nyuki na maua mazuri.

Mlusina hufananishwa na mkunde mwingine (alfaalfa) muhimu kwa wingi wa virutubisho haswa protini kwa ajili ya mifugo. Lakini Mlusina una upungufu wa sodium na iodine lakini una wingi wa b -carotene.

#HifadhiMitiKwaFaidaYaTaifa
 
Isee naujua huu. Hapa jirani yangu kakata mwembe mkubwa wenye zaidi ya miaka 30 kuna watu wana ugomvi na miti imenikela sana
 
Isee naujua huu. Hapa jirani yangu kakata mwembe mkubwa wenye zaidi ya miaka 30 kuna watu wana ugomvi na miti imenikela sana
Ase miti ni muhimu sana, inafaa kwa kutunzwa na si kukatwa kwani kama upo mahali sahihi na unaleta faida kwa wengine si vema sana kuukata ama kuuharibu.
 
Tuna weza kujenga uadui maana wote ni wakazi wa kudumu. Ulikua na faida watoto wanakula embe na tulipata hewa safi
lilikuwa jambo zuri sana. sio vibaya mkuu kama ukichukua hatua kupanda mti mwingine kama huo uliokuwepo ili watakaokuja baadae wapate hiyo hewa safi pamoja na matunda.
 
mkuu,
unaweza toa mbao ambazo zinaweza kutumika kwa muda mfupi kujengea au mrefu kuezekea ikiwa utawekewa vitunzifu.

Mimi ninazo mbao za mti huu.Kama mti wa lusina umemaliza miaka 15 na zaidi mbao zake ni ngumu mno na hazipekechuliwi na wadudu hata mchwa tu anashindwa.Mbao zake zikikauka misumari haipiti kiurahisi
 
Mimi ninazo mbao za mti huu.Kama mti wa lusina umemaliza miaka 15 na zaidi mbao zake ni ngumu mno na hazipekechuliwi na wadudu hata mchwa tu anashindwa.Mbao zake zikikauka misumari haipiti kiurahisi
sawa sawa inawezekana, na haujawekwa dawa mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…