Ufahamu Mti wa Mlusina (Leucaena leucocephaela)

Ila hapo kwenye asili yake napata shaka. Nimeiona hiyo miti porini huko sana tu!
kuwepo huko porini hakumaanishi umekuwapo huku kwetu miaka mingi au ndio asili yake la hasha bali inawezekana uliletwa nchini then ndo ukasambaa au watu wakafika nao hadi hayo maeneo.
kwa mfano mti wa pinus asili yake ni nje lakini upo sana katika mlima rungwe kama mti vamizi, so pia unaweza ukahisi umeanzia au kuzaliwa huko lakini sivyo.
 
Mlusina ni mti wa kigeni kama ulivyosema na kiukweli hapa TZ iliingizwa hasa hasa kwa kilimo mseto, sijawahi kuona umetumika kama mbao.
mkuu,
unaweza toa mbao ambazo zinaweza kutumika kwa muda mfupi kujengea au mrefu kuezekea ikiwa utawekewa vitunzifu.
 
Aya tuelekezane jinsi ya kuandaa iyo mboga vipi inawekwa nyanya au vitunguu sammu, na inaliwa na ugali au
 
sawa kabisa mkuu, mti anaosema jamaa haponi huu
Mkakaya (Delonix regia) ambao hutoa maua mekundu.

View attachment 1075199

wakati mlusina unatoa maua meupe.

View attachment 1075201
Naona umeweka na scientif name yake kabisa. Hongera. Nilikuwa najua english name na scientific lakini kiswahili nilikuwa sijui.

Halafu huu mti umeitwa mkrismasi kutokana na kugongana kwa msimu wake wa kutoa maua kwa ukanda wetu ambao ni mwezi December.

Kanda nyingine maua huchipua vipindi tofauti tofauti vya mwaka
 
Aya tuelekezane jinsi ya kuandaa iyo mboga vipi inawekwa nyanya au vitunguu sammu, na inaliwa na ugali au
hahaha.. unaeka kitunguu tu na mafuta kidogo sana. lakini wanadai ina keikali ya mimosine ambayo ina asili ya sumu hivyo matumizi yake si salama sana mkuu (risky).
 
ni kweli kabisa mkuu. asante kwa elimu hiyo.. maua yake yanavutia mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…