Ufahamu mwanzo wa jeshi la KAR (Kings African Rifle) ambalo ndilo mama mzazi wa JWTZ/TPDF Tanzania,KDF Kenya,UPDF Uganda na baadhi ya vikosi Afrika

Ufahamu mwanzo wa jeshi la KAR (Kings African Rifle) ambalo ndilo mama mzazi wa JWTZ/TPDF Tanzania,KDF Kenya,UPDF Uganda na baadhi ya vikosi Afrika

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Jeshi la KAR ( kings African Rifle) ni jeshi ambalo limeanzishwa na kutoholewa kutoka kwenye makundi mabalimbali ya maaskari wa Kiafrika mnamo mwaka 1902. Jeshi hili lilianzia Afrika ya Mashariki ambayo kwa kipindi hicho ilijumuisha Kenya,Uganda,Tanganyika na Nyasaland /Malawi ya sasa.Lengo la kuanzishwa kwa jeshi hili lilikuwa ni kusanifisha mafunzo na utendaji kazi wa maaskari hao katika kuitumikia serikali ya Wakoloni

Lengo lao kubwa lilikuwa ni kurahisisha utendajikazi wa maaskari hao na wawe na majukumu yanayofanana.

Mwanzo kabisa lilianza likiwa na vikosi sita (6) na mpangilio wa vikosi hivyo ni pamoja na
1st Nyasaland Batallion 1902-1964 na
2nd Nyasaland Batallion 1902-1963
∆ Vikosi hivi vilifahamika pia kama CENTRAL AFRICA BATALLIONS yaani Vikosi vya Afrika ya Kati.


3rd KENYA Batallion 1902-1963
4th Uganda Batallion 1902-1962
5th Uganda Batallion 1902-1904
kikosi hiki ni kikosi ambacho kilikuwa kwa kasi mno kuliko vikosi vingine vyote na pia ndicho kikosi cha kwanza kuanzishwa.
6th Somaliland Batallion 1902-1910
Hii ilihudumubzaidi na kufanya kazi zake kwenye Somalia ya Kiingereza.

Mwaka 1902 walipoanza walikuwa na jumla ya askari wazungu 104 ambao walikuwa ni maafisa na waafrika 4,579.Idadi ya maaskari vikosinibilioungua baadaye baada ya maafisa kutaka kuwa na idadi kubwa ya maaskari wenye elimu juu ya matumizi ya silaha kama ilivyo leo ambapo huwezi kuwa askari kama hujasoma katika Taifa letu la Tanzania na mataifa mengine Afrika na duniani.
Ni kweli na ni wazi kwamba leo JWTZ hawaajiri watu ambao hawana hata elimu ya msingi yaani basic education.Siyo wao ndiyo walioanzisha,hapana hii ilianzia mbali na kanuni hii ilikuwepo tangu utawala wa wakoloni.

Kumbuka kwamba Batalion ya Tanganyika haikuwepo kwenye huo mpanglio kwa kuw ilianza baadaye sana mjerman alipoidondosha mwaka 1918 baada ya vita vya kwanza vya dunia vya 1914-1918 ndipo tukapokelewa na Muingereza tukawa Territory ya British chini ya uangalizi wao hata tulipojitambua wakatuachia uhuru..... JWTZ ilianzishwa Septemba 1964 baada tu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kamanda wa kwanza akawa ni mh Mrisho Sarakikya..

Mungu ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki JWTZ/TPDF
JAMBO AFANDE.
 
Jwtz ilianzishwa baada ya maasi ya mwaka 1964 ambapo mkuu wa nchi enzi hizo alipoamua kulivunja jeshi alilorithi kutoka kwa mwingereza na kuunda lake akisaidiwa na baadhi ya nchi za kigeni.
 
Back
Top Bottom