Ufahamu wa baadhi ya Watumishi wa umma ni mdogo, Kauli ya huyu mtumishi mwenzangu imenishangaza

Ufahamu wa baadhi ya Watumishi wa umma ni mdogo, Kauli ya huyu mtumishi mwenzangu imenishangaza

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari wakuu!

Jumatatu nikiwa ofisini katika stori za hapa na pale Mzee mmoja ambaye ndiye mkuu wa kitengo chetu au boss wetu akajikuta ametamka neno.

Alisema hivi "Magufuli akiongeza mshahara mwezi huu( October) tutamwagia kura mpaka ashangae".

Kila mmoja anajua kuwa watumishi wa umma hawajaongezwa mshahara kwa miaka mitano mfululizo kwasababu ya Maendeleo( madaraja, umeme, hospitali n.k). This is according to President Magufuli.

Sasa mwezi Octoba itokee Magufuli ameongeza mshahara ndio iwe sababu ya kumwagia kura?.

Kama sababu ya kutopandisha mshahara ni Maendeleo ya miundombinu, je, ujenzi wa miundombinu sasa umekamilika?.

Je, mshahara ni hisani?.
Je, fidia ya ugumu wa maisha aliyopitia mtumishi wa umma kwa miaka 5 itawekwa kwenye hesabu ipi?.
 
Back
Top Bottom