Ufahamu Wa Mahusiano Na 'Red Flags'

Ufahamu Wa Mahusiano Na 'Red Flags'

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Watu wengi tumekuwa tukipuuza ishara mbaya katika mahusiano yetu, lakini tambua kwamba mwenzi unaemshahili atakuwa vile unahitaji.
Wanawake wengine siku hizi wamekuwa wakisema wanateswa na kuendeshwa na mwanaume, kwasababu hawajui wajibu wao kwa mwanaume huyo, pale unapomuomba mpenz wako kuwa hupendi tabia ya matumizi ya simu yaliopitilia anakujibu "Simu si yangu, kwann sina uhuru nayo". Majibu haya hukwaza hasa pale unapomuambia kwa upendo ila akajibu kwa namna hii.

a-couple-arguing-in-silhouette.jpeg



Red Flags...
Sio Kila ishara Mbaya ni mbaya, lakini zipo ambazo huepukika na kuzuilika, Kabla ya kuchukulia ishara kuwa mbaya jaribu kufikiria nani msababishi?, Je zote hutokea hivyo?, Je wewe unahusika hivi hadi mtu kuonesha ishara mbaya?, Kwa7bu unaweza mkwaza mwenzi wako akashindwa zuia hasira zake hiyo haimaanishi hiyo ni 'Red Flag' bali ni mgogoro, kwasababu wewe ni chanzo cha yeey kukosa Udhibiti wa hasira zake.

Ishara mbaya ni zile tabia za mtu ambazo hujionesha hata bila 7bu ya msingi, mfano unamuelekeza mpenzi wako sipendi hivi, wacha hivi lakini akakifanya hiyo ni ishara mbaya kwa7bu ameshindwa kufata maelewano na ww ukikosa udhibiti wa hasira hauwi mbaya bali umesukumwa kuwa mbaya. Ishara Za Hatari huwa zinatokana na tabia za mtu mfano Kiburi, ni kitu ambacho huweza fanyiwa hata kwa mtu asie mpenz. Tujifunze kuyaishi mahusiano yetu katika hekima na busara.
sadpersonas-risks-symptoms-suicide-1170x585.jpeg

Tujifunze kujishusha, kwa wale wapenz ambao wamepishana kauli na kila mtu akatoa hasira zake kwa namna yake, wapo ambao huongea sana wanapopata hacra, wapo ambao kususa, wapo ambao hukaa kimya, wapo ambao hukuta tamaa, wapo wanaopiga. Lakini unapotambua mlikwazana au ulimkwaza mtu hadi kuonesha hasira zake kujishusha ni hekima na sio utumwa, EGO na Kiburi Na Kiona kutakuja kufanya upoteze watu ambao wangekufikisha mbali sana.

Wanawakeee...
muelewe kitu kwamba mwanaume anapokuambia uache kitu fulani basi wacha ili kuepusha kukwazana na mwanaume afanye same, Kwa sababu ili muwe na future yenye furaha basi ni hekima mkapita njia moja, mnapoishi vile kila mtu anavyotaka basi hamuwezi kufika mbali kwa7bu kila mmoja atakuwa na mtazamo tofauti, na kujikuta mkiangukia katika migogoro na mifarakano isiokuwa na lazima

tujifunze kuwa na mikakati katika mahusiano kwani kila mmoja alishapia mahusiano anayoyajua yeye na amezoea alivyozoea yeye, ivyo ukiishi kwenye mahusiano kwa namna wewe ulioizoea huenda isiwe sawa na mwenzi wako, hivyo ni vema kuishi kwa maelewano na kusikilizana, kumtii mpenz wako sio utumwa ila ni kuepusha migogoro isiofaa, akikukataza wacha pombe, marafiki wasiofaa usione anakunyima uhuru ila anajaribu kukufanya kuwa bora kwaajili yake.

mahusino yanayodumu kwa muda mrefu na yenye furaha ni yale ambayo wapenz wameelewana na kushauriana vizuru namna ya kuishi katika pamoja ili kuweka mbali mazoea na vijitabia ambavyo kila mmoja kavizoea.
happy-relationship-1024x575.jpeg
 
Uko sahihi mkuu.
Personally nimewahi soma kitabu kinaitwa " THE UNPLUGGED ALPHA' ( the no bullshit guide To winning with women and life.

Mwandishi amelezea mambo mengi sana hasa Kwa sisi wanaume .
Huku akielezea mifano michache (Red flags ) ambayo UKIONA mwanamke wako anazo kimbia haraka sana .
-
 
Uko sahihi mkuu.
Personally nimewahi soma kitabu kinaitwa " THE UNPLUGGED ALPHA' ( the no bullshit guide To winning with women and life.

Mwandishi amelezea mambo mengi sana hasa Kwa sisi wanaume .
Huku akielezea mifano michache (Red flags ) ambayo UKIONA mwanamke wako anazo kimbia haraka sana .
-
Shida Ya sisi huwa Tunajipa moyo kuwa ipo wakati atabadilika, alafu inakuja kuwa tofauti, unajikuta unaumia na kujutia
 
Back
Top Bottom