Top gun maverick
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 2,080
- 2,871
Habari wapendwa wa jamii forums Kwanza nipende kutoa shukrani kwa mawazo yenu mazuri ya kujenga au kutoa ushauri mzuri kwa mtu.Husika na kichwa cha habari hapo juu Mimi Ni kijana Nina umri wa miaka 21. Nilibahatika kupata bahati ya kwenda chuo.na kupata bahati ya mkopo (boom).Awali nilikuwa na mipango mingi Sana kwamba nitajitahidi niwe na save kidogo kidogo ili niweze fanya biashara Kama vile mpunga,mpesa au kufuga kuku.Lakini vice versa is true nimepokea almost 2million na ushee.lakini nothing done,sasa npo likizo sina hata Mia.ningependa kuomba ushauri nawezaje kuwa na financial discipline..au nifungue fixed account,au Kuna namna nyingine ya kusave hela ya akiba kidogo kwa sababu pesa Ina lugha moja inasema.."if you save me today I will save you tomorrow"...natanguliza shukrani Asante!