Ufalme na u-mungu mtu wa clouds unasimikwa na wasanii wenyewe

Hans makini

Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
59
Reaction score
29
Kwenye wimbo wa Bongo Hip Hop wa FidQ kuna mstari unasema hivi:-

"Sio tu BONGO mpaka NG'AMBO hakuna UHURU wa HABARI... kuna uhuru wa mwenye CHOMBO, MITAMBO na mwenye MALI... Kujifanya hawasikii, haiwasaidii, wala HAIWAJENGI... Unachosema ni kamwe IPP haitompinga Mengi."

Mstari huu unanifunza kwamba huu uhuru unaoliliwa sana na wasanii wetu ni ngumu sana kupatikana ama hata kuuona tu sababu dunia nzima uhuru upo kwa mwenye chombo, mitambo na mali na huu ndo ukweli ambao ni ngumu sana kuukubali.

Lakini kabla ya kuanza kuvilaumu hivi vyombo vya habari Serikali yetu kupitia sekta za sanaa wao wanamitazamo ipi juu ya hizi sanaa? Je haya malalamiko yanayotolewa na wasanii kila mara wao hayawafikii? Na kama yanawafikia huwa wanayaweka kwenye droo za meza zao tu (kupuuza)? Au bado wanayatafutia ufumbuzi? Lakini pia hizi taasisi (Wizara ya Habari, michezo na BASATA) zinaSERA zenye mwongozo wa kuielea sanaa ya Tanzania? Haya ni maswali ambayo miye binafsi najihuliza.

Tatizo lingine wasanii wetu wa Bongo chombo cha habari wanachokipa thamani na kukitumainia ni Clouds fm pekee, yaani ni bora redio zote zisipige wimbo/nyimbo yake/zake ila ukipigwa Clouds tu kwake ni faraja tosha. Nyimbo za Diamond EAST Africa Radio hawapigi ila sijawahi kusikia meneja wa Mond kutoka hadharani na kuwanyoshea vidole ya kwamba kwa nini hawapigi nyimbo za Mond, ila kutopigwa kwa Clouds tu wamekuja juu, hapa najifunza kuwa ufalme na huu tunaouita U-Mungu mtu wa Clouds unapandishwa na WASANII WENYEWE.

Clouds fm wapo vizuri kwenye suala zima la kutoa 'PROMO' kwa wasanii hivyo wanauwezo mzuri wa kumpandisha msanii na kumfanya hajulikane hilo ni ngumu sana kupingwa, sasa ukikubali kubebwa kinachofuata ukubali na kushushwa. Kwenye wimbo wa hawatuwezi wa Nako 2 Nako Lord Eyes anasema;

"Yule yule anayekupandisha ndo yule atakayekushusha"

Bahati mbaya au nzuri Mond Clouds walimbeba wakati anaanza lakini leo hii Mond anajibebesha ama kujibeba mwenyewe hivyo ni ngumu sana kumshusha sababu hujui amejibebeshaje mpaka kufika hapo halipo. Lakini kwenye wimbo huo huo wa hawatuwezi Lord Eyes anasema tena;

"Macho kwenye fedha dizaini ya mbwa msaka fedha... Huu sio mchezo ni vita na hivi ndo tunavyovicheza"

Kwenye huu mstari namuona DIAMOND kwa namna anavyozitazama fedha kwa jicho la uchu, kwa namna anavyoumiza akili kuzitoa pesa zilizo ndani ya kichwa chake na kuzileta kwenye uhalisia wa makaratasi wakati anayafikiria yote haya anatambua kuwa mafanikio yake hayaletwi kwa dhana rahisi ya uwanja wa buradani ila anaamini yupo kwenye uwanja wa vita na ni lazima apambane vilivyo ili aweze kufanikiwa / kushinda.

Kikubwa zaidi na chenye uungwana ni Ruge kupambana na hali yake na Sallam na Team yake wapambane na hali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…