Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ufalme uliogawanyika wenyewe kwa wenyewe hauwezi kusimama. Usemi huu una maana gani kwetu kama taifa? Je tunaweza kukaa na kutafakari kuhusu usemi huu? Nawaomba tukae na kufikiria kwa makini usemi huu. Ambao ni muhimu sana. Nguvu yetu kama taifa itategemea sana kama tutauelewa usemi huu. Na ukweli ni kwamba mataifa mengine hufurahi kuona mataifa mengine sio wamoja kwasababu wanajua kwenye umoja kuna nguvu. Kama watu wakiamua kujenga taifa lao kwa pamoja na kwa sauti mmoja hawawezi kushindwa. Ni muhimu kuwa na sauti moja kama tunataka kujenga taifa hili.
But Our generation is the generation of the self seekers and not of nation builders.
But Our generation is the generation of the self seekers and not of nation builders.