Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kiwango cha ongezeko la maandamano nchini Jordan kumeanza kutishia ufalme wa nchi hiyo.Wiki iliyopita waandamanaji hao walifurika mitaani na kuzunguka ubalozi wa Israel.
Pamoja na kubeba mabango ya kusifia wapiganaji wa Hamas,waandamanaji hao walisikika wakiimba kuwa wao ni wafuasi wa Yahya Sinwar ambaye anakisiwa yuko chini kwenye mahandaki ya Gaza ambako Israel imeshindwa kumfikia.
Baadhi ya vichocheo vya ongezeko hilo imetajwa ni msimamo wa waziri mkuu wa nchi hiyo ambaye amekuwa akitoa matamshi makali dhidi ya Israel na pia mke wa mfalme Abdalla ,bi Rania ambaye bila kizuizi amekuwa akitoa matamko ya kizalendo.
Mmoja ya viongozi wakuu wa Hamas aitwaye Meshaal ni raia wa Jordan na hotuba zake zimekuwa zikiungwa mkono sana nchini humo ambapo kuna Idadi kubwa ya watu wa Gaza ukongezea na wapalestina w maeneo mengine.
Miaka michache iliyopita ufalme huo uliponea chupuchupu kupinduliwa na wanamapinduzi ambao waliungwa mkono na Iran na Syria.
Iwapo ufalme huo utapinduliwa na madaraka kushikwa na watu wenye misimamo ya Hamas na Ikhwanul muslimina itakuwa ni tiketi kubwa ya wapalestina kurudi kwenye ardhi zao zinazokaliwa na Israel tangu mwaka 1948.