Ufanisi wa wafanyakazi Serikalini na nyongeza ya mishahara yao

Ufanisi wa wafanyakazi Serikalini na nyongeza ya mishahara yao

Ndinani

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
7,329
Reaction score
4,286
Rais Magufuli alipoingia madarakani kitu cha kwanza alichojitahidi kurekebisha ni jinsi wafanyakazi wa serikali walivyokuwa hawawajibiki kutimiza majukumu yao; alifanya zoezi la ziara za kustukiza maofisini na kuwaadhibu wale waliokutwa na makosa.

Zoezi la ziara za kushstukiza pamoja na zoezi la kuwatumbua wale waliokuwa na vyeti vya kazi bandia lilileta muamko kwa wafanyakazi kujali wajibu wao na hivyo kuleta sifa kwa Magufuli kuwa aliweza kuwafanya watumumishi wa serikali kuwajibika.

Kwa bahati mbaya sana ufanisi wa wafanyakazi uliopatikana ulikuwa wa muda mfupi sana kwani hali imerudi kama zamani. Unakwenda kwenye ofisi za serikali huduma ni duni na ule mtindo wa file kupoteza kama shinikizo la kuomba rushwa umerudi tena!!

Yote hii Inawezekana ni kwasababu ya serikali kutokujali maslahi ya wafanyakazi kwa muda mrefu; pia hawa maDc na maRc kupoteza muda mwingi kutafuta media attention kwenye television badala ya kuwasimamia watumishi wao kuhakikisha kuwa wana timiza wajibu wao!

Mimi ni muhamga wa utumishi mbovu pale idara ya ardhi wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Ni takribani miaka mitatu sasa nafuatilia title deed lakini bado napigwa Dana Dana; hata pale mkuu wa wilaya alipoingilia bado wanasuasua kunitayarishia title ingawa nimekwisha lipia ada zote na kuwapa vilelezo vyote vinavyohitajika.

Sasa nashawishika as a last resort kwenda Takukuru kufikisha malalamiko yangu pengine wakipewa hela za moto watashika adabu.
 
Back
Top Bottom