GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
habarini wana JF, nimeamua kuanzisha hii thread maalum ili tuweze kupeana INFORMATION za mikoa mbali mbali kwani wana JF wanatoka mikoa tofauti. Mfano nataka kujua aina gani za biashara ni nzuri katika mkoa wa Dodoma. Unaweza kutueleza kuwa biashara ya Majaketi ni nzuri zaidi katika mkoa wa Dodoma (Kwa wauza nguo) Mtwara unaweza kufanya biashara ya samaki hasa wale wakavu wanaotoka Mwanza wana soko zuri sana kule lakini ni Katika wilaya zake si pale mkoani.
Unaweza kutueleza kuwa mahitaji ya chumvi kwa mkoa wa Ruvuma ni makubwa sana sina uhakika kwa sasa lakini nakumbuka miaka ya nyuma Songea chumvi ilikuwa bidhaa yenye soko zuri. Mwaka jana nilikuwa mkoa wa Mtwara biashara ni nzuri kuanzia Mwz 10 mpaka FEB. Pia nilivuka mpaka kwa njia za panya na kwenda msumbiji Dawa za mimea na mifugo zinapatikana kwa bei nafuu sana kule! Mfano MUPAFIDAN(ya kuulia wadudu kwenye mimea) nilinunua kwa sh 3,000 nikaiuza Mtwara kwa sh 12,000 na nasikia bei yake ni kubwa zaidi DAR. Tupeane INF. za mikoani NAWASILISHA.