Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kuna watu ambao huwa na tabia ya dharau, majivuno, kiburi, ujuaji,wanajiona ni wazuri sana,wanajiona ni ma-superstar kwa maana ukiwa naye kwenye mahusiano akili yake inaamini kwamba anakusaidia kuwa na wewe kwa maana anataka kukuaminisha kwamba upo na bahati kubwa sana kuwa naye kwenye mahusiano.
Watu wengi wenye hulka hii huwa na marafiki wengi sana lakini wakiwa na matatizo huwa wanakwenda kuomba msaada kwa watu ambao wao waalikuwa wanawaona kama takataka,kuwaona kama laana.
mambo ya kufanya pale ambapo Mwenza wako anakupuuza sana
1.ACHA KUMTAFUTA
Kama unaona unatumia nguvu nyingi sana kupata attention yake,acha kupiga simu mfululizo au kutuma sms mfululizo ili kulinda heshima yako
-Acha kumtafuta mwenza wako kama anatumia masaa kadhaa au siku kadhaa kujibu sms zako lakini wakati huohuo anakuwa anapokea simu haraka za watu wengine na anajibu haraka sms za watu wengine.
-Kama mwenza wako hafanyi juhudi zozote za kukutafuta mpaka uanze wewe,kama haelezi sababu za kukaa kimya muda mrefu sana,kama ukiuliza kuhusu mabadiliko ya tabia zake anakuja juu kwa jazba,anaporomosha matusi ya nguoni, anakufokea, anakujibu vibaya, hakusikilizi, anakudhalilisha,anaakushambulia kwa maneno makali sana.
-Kama huwa anatafuta kisingizio cha kukata simu kila wakati unapomtafuta,kama huwa anaanza kukulaumu kwa sababu ya ukimya wake,kama huwa anakupa kashfa za uongo na tuhuma za uongo kama kisingizio cha kuficha tabia zake.
2.ACHA KUFANYA UWEKEZAJI WOWOTE KWAKE
Kosa kubwa ambalo unaweza kufanya ni kutumia fedha nyingi sana,ili ubadilishe maisha ya mwenza wako labda kwa kumsomesha lakini akiwa masomoni anakuwa busy sana,anakuwa mkali kupitiliza kila unapohoji mabadiliko ya tabia zake
-Anakuwa mkali kupitiliza kila unapotaka muonane, wakati huohuo unamjengea,anakuja kwako akiwa na matatizo tu lakini baada ya kumsaidia anaondoka mpaka uanze kumtafuta
-Epuka kumfungulia biashara kwa sababu akiwa vizuri kiuchumi tu atakugeuka ghafla atasema wewe sio wa HADHI yake
-Epuka kumnunulia zawadi za gharama kubwa kwa sababu zawadi hizo atakwenda kuhonga wanawake au wanaume ambao hawana malengo naye wala hawana msaada wowote kwake
-Epuka kujinyima chakula ili yeye ale,epuka kupauka ili yeye ang'ae,epuka kuhatarisha uhai wako ili uthibitishe kuwa ûnampenda sana kwa sababu atakuona bwege na mara kwa mara atakuwa na uhakika kwamba hauwezi kuishi bila yeye wala hauwezi kumuacha tatizo hili linaweza kumfanya akudhalilishe mara kwa mara
-Epuka kumsaidia kukabiliana na matatizo yake kwa sababu atakuwa anakuja kwako akiwa na matatizo tu lakini anakuacha ghafla bila sababu zozote za msingi
-Akijitenga na wewe jitenge naye, akikupuuza mpuuze, akikaa kimya kaa kimya,akikuona kitu cha ziada muone kitu cha ziada,kama hana muda na wewe acha kutenga muda kwa ajili yake.
3.FANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA KWAKO
Kula vizuri, vaa vizuri, tumia manukato mazuri,jipe zawadi,toka "Out",Kutana na watu wapya mara kwa mara, jifunze vitu vipya kila siku unapokuwa mpweke
-Tumia 90% ya fedha zako na muda wako kujali malengo yako.Kama utafungua biashara, kujenga,kuongeza elimu yako,hauwezi kuumia kama mahusiano yamevunjika.
Utaumia sana kama alikuwa na ujauzito au watoto wa wanaume wenzako lakini ulijitoa mhanga kumfariji, kumliwaza, kumtetea ili akuone ni husband material
utaumia sana kama umemlipia ada masomoni lakini baada ya kuhitimu masomo akasema wewe sio wa HADHI yake
utaumia sana kama umemfumania na mtu mwengine kwenye nyumba ambayo umemjengea,
utaumia sana kama umepauka ili yeye ang'ae,utaumia sana kama umekonda sana ili yeye ale vizuri
utaumia sana kama amekusaliti au amekuacha ghafla ukiwa mgonjwa sana, au hauna kazi wala biashara yoyote,au umekonda sana au umepauka sana .
Angalia mfano huu.
Kama umetumia pesa nyingi sana kumjali sana mwenza wako utakuwa unampa uhakika wa 100% kwamba endapo akiondoka kwenda kwa Watu wengine akitaka kurejea kwako utampa nafasi nyingine.
Mtu yeyote anapotaka muachane lakini baadaye arudi kwako huwa anaibua ugomvi ghafla kisha anakuangalia.
Akiona unambembeleza sana,unalia, unapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kupiga magoti, kutishia kujiua,akiona unakosa amani na utulivu atajaribu kuondoka kwenda kwa mwanamke au mwanaume mwengine akiona unapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kulalamika kuumizwa,kumuomba msamaha anakuwa na uhakika kwamba kama mahusiano yatavunjika huko kwenye penzi jipya anaweza kurudi kwako na kupata mapokezi mazuri.
Watu huwa wanajua kama wanapendwa sana pale ambapo wanakujibu vibaya lakini unaomba msamaha,au ananuna atasusa, atakaa kimya mara kwa mara,anakujibu vibaya lakini anakuona unahangaika kutaka kumfurahisha hapo anajua kwamba ûnampenda sana hivyo anakuwa na uhakika kwamba hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Mtu yeyote akijua anapendwa sana kiburi huanza kujitokeza lakini kama mtu amekupuuza halafu anaona haupotezi hata sekunde kumfuatilia anajua kwamba haumpendi.
Mwanaume au mwanamke anapotaka kukupima kama ûnampenda sana anaweza kukuupuuza kwa makusudi kisha akiona hauna muda wa kumfuatilia kwa chochote ataanza kukulaumu kwamba haumpendi.
Mtu yeyote akionyesha kukuupuuza acha kumsumbua ili kiburi kiondoke.
Kiburi , majivuno, jeuri na dharau hujitokeza pale ambapo mtu anaona unambembeleza sana wakati huohuo yeye anakuonyesha dharau kwa makusudi.
Tumia muda mwingi kujali afya yako, kula vizuri,kuvaa vizuri,kujali malengo yako.
Malengo yako yape kipaumbele zaidi pale ambapo Mwenza wako anakupuuza.