Ufanyeje Unapokuwa Umekosea katika Biashara?

Ufanyeje Unapokuwa Umekosea katika Biashara?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;
Katika biashara kuna kukosea.Hii ni kama ilivyo katikamaisha ya kawaida.Kukosea ni sehemu ya ubinadamu.Kila kosa huwa lina gharama na matokeo.Haya yanaweza kuwa mabaya sana au ya wastani.Katik biashara makosa huweza kupelekea hasara katika biashara,kupoteza mteja na hata kufa kwa biashara yako.

Katika kuendesha biashara makosa mengine yanaweza kuwa nje ya uwezo wako na mengine yanaweza kuwa ndani ya uwezo wako.Makosa mengine tunaweza kufanya kwa kujua kabisa kwamba ni makosa na kujipa moyo kwamba madhara hayatatokea.Makosa mengine tunaweza kufanya kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi kwa wakati sahihi.Yote kwa yote kukosea kupo.Na biashara nyingi zinaathiriwa na makosa ya kila siku yanyaofanywa na wamiliki,wasimamizi au waajiriwa.

Leo nimeona nilete mada ya kujadili Juu ya kila ambacho unaweza kufanya kama mjasiriamali iwapo utafanya makosa katika Biashara yako au mradi.Mjadala huu ni wawazi na kila mmoja wetu anaweza kutoa maoni yake na nitakayoyaweka hapani baadhi tu ya mambo ila mengi yapo katika experience za wengi waliopo katika biashara.

Badhi ya makosa unayoweza kufanya katika biashara ni pamoja na makosa katika maamuzi ya mradi wa kufanya,makosa katika kuajiri watumishi,makosa katika matumizi ya rasilimali,makosa katika kuhudumia wateja,makosa katika kuweka mikakati na mipango.Makosa haya yote hufanyika katika biashara kubwa na ndogo na haijalishi ukubwa wa biashara makosa haya huwa na athari katik utendaji na mafanikio ya biashara.

Inapotokea umefanya katika biashara yako USIOGOPE.Sio mwisho wa dunia na wala wewe sio wa kwanza au wa pekee kufanya kosa kama hilo.Wengi walishanyanya makosa na hakun kosa ambalo halina suluhisho.Hivyo basi kitu cha kwanza ni kuondoa hofu na WOGA na kulitazama KOSA katika mtazamo sahihi.

Baada ya kuondoa hofu hatua ya pili na kulipima KOSA kwa kutazama madhara yake kwa biashara yako.Hapa tazama madhara ya muda mfupi na ya muda mrefu.Kumbuka katika biashara unapoangalia madhara angalia jinsi ambavyo yanavoathiri kiwango cha MAPATO,MATUMIZI na FAIDA katika kipindi cha muda mfupi,wa kati namuda mrefu.Kwa nini nasisitiza hili la kutazama Mapato,Matumizi na Faida?Ni kwa sababu hayo ndio maeneo ya muhimu ya kutazama katika biashara.

Ukisha Tazama athari zake na kuona kiwango cha madhara yanayoweza kutokea JIulize iwapo biashara yako inao uwezo wa kumudu kiwango cha madhara yatakayotokea.Jiulize Je kwa haya madhara aambayo ninayaoa Je biashara yangu bado itaweza kuendelea kujiendesha hata kwa faida kiduchu.Hapa ni lazima kuweka hisia pembeni kwani mjasiriamali yeyote huwa na mahaba na biashara yake na ni vigumu kwa yeye kuamini na kukubali kwamba biashara yake "lost cause"

Ukishatambua athari na uwezo wa biashara kuzistahimili hatua inayofuata ni kufanya uamuzi wa nini cha kufanya.Kwa mfano unaweza kuamua kuendelea na biashara au mradi na kufanya maboresho na marekebisho au unaweza kusitisha kabisa biashara au mradi husika.Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba hauingii katika mtego unaitwa "Sunk cost Fallacy" kwa kufikiria kwamba kiwango ulichowekeza ni kikubwa na unataka urudisha hela yako kwani kwa kufanya hivyo unaweza kuendelea kupoteza zaidi.

Vyovyote vile utakavyoamua ni muhimu sana ukatumia makosa uliyofanya kama fursa ya kujifunza hasa kwa ajili ya maamuzi na uzoefu wa baadae.Ni muhimu ukajiuliza maswali 5 ya kwa nini ili kufanya kitu kinaitwa "root cause analysis" Utafiti wa chanzo cha tatizo.Hii itakusaidia kuepuka kurudia makosa hayao katika mazingira hayo au mazingira tofauti.

Je wewe huwa unafanya nini unapogunda kwamba UMEKOSEA katika BIASHARA yako?

Tujadili na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto za biashara.
 
Back
Top Bottom