MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Leo nipo upande wa Congo. Nawasalimu kwa jina la Bolingo.
Nimesikitishwa mno kusitishwa kwa Show ya mwanamuziki Werrason akiwa na kundi lake la Wenge Maison Mere. Show ilikuwa ifanyike tarehe 25/09/2021 kwenye ukumbi wa Zenith, Paris. Wakati wote wa maandalizi kundi linalojiita Combattants lililopo karibu Ulaya nzima lilitishia kuzuia kutofanyika kwa show hiyo.
Combattants ni kina nani? Hawa ni wacongo wanaoishi Ulaya huku wakipinga serikali ya DRC. Walianza kwa kuipinga serikali ya Joseph Kabila lakini wameendela kupinga hadi utawala huu uliopo kwa sasa. Sasa kwanini wanazuia wanamuziki wa Congo kupiga show Ulaya? Wenyewe wanadai wanamuziki wako upande wa serikali huku wakinufaika bila kujali mateso wanayopitia wacongo wengine. Combattants wenyewe wanaona wanamuziki ni sehemu ya maadui zao kwa maana ya serikali. Uzuiaji wao umefanikiwa na kuwaathiri mno wasanii wa Congo. Kwa zaidi ya miaka 10 imekuwa ngumu kwa mcongo kupiga show Ulaya.
Juzi serikali ya Ufaransa kupitia jeshi la polisi lilitoa Tamko la kusitisha show ya Werrason kufuatia kuwepo taarifa za kiitelijensia kuwapo kwa combattants wataovuruga amani. Ikumbukwe Karibu mwaka mzima kumekuwa na maandalizi ya hiyo show ambayo ilivuta hisia za mashabiki waliokuwa na kiu kali ya rhumba toka kwa mkongwe Werason. Tiketi zilinunuliwa online. Tayari werrason kaanza kurudisha viingilio.
Binafsi naitupia lawama serikali ya Ufaransa kushindwa kudhibiti kikundi kidogo cha wahuni wanaojiita Combattants. Hiyo ni nchi yenye miguvu ya kutosha kila idara. Kutoa tamko la kushindwa ni kama hujuma dhidi ya Werason pia ni kuonyesha wazi kutotaka mwafrika mwenzetu kupiga show pale Zenith. Wangewaazima hata polisi wetu wakatoe kipigo kitakatifu kwa hao Combattants. Kwasababu tayari Combattants wametoa onyo kwa mwanamuziki mwingine kutoka Kinshasa anayejulikana kama komredi Koffi Olomide na kundi lake la Quartier Latin International kwamba watazuia onyesho lake analotarajia kufanya November kwenye ukumbi wa U-Arena, Paris wenye uwezo wa kuchukua watu 40,000, basi ni vema polisi wakawadhibiti toka muda huu. Ingekuwa hapa kwetu hao viongozi wa Combattants wangeshapewa kesi mbaya mbaya zisizo na dhamana. Pia wafuasi wao wangepata kipigo cha mbwa koko.