Ufaransa yashika namba moja katika viwango vya FIFA, Tanzania yawa ya 140

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Timu ya soka ya Wanaume ya Ufaransa imefanikiwa kushika namba moja katika orodha ya timu bora za Dunia iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka la Dunia(FIFA)

Ufaransa imefanikiwa kushika nafasi hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tangu watwae Kombe la Dunia nchini Urusi

Aidha, Ujerumani ambayo ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe la Dunia yenyewe imeshika nafasi ya 15 huku Argentina ikiwa nafasi ya 11 na Uhispania ikiangukia nafasi ya 09

Katika orodha hiyo Tanzania inashika nafasi ya 140 huku nchi ya Kwanza kwa Afrika ikiwa ni Tunisia ambayo inashika nafasi ya 24 kidunia

Kwa bara la Afrika, Tunisia imelingana alama na Senegal zote zikiwa nafasi ya 24 zikifuatiwa na Congo(37), Ghana(45) na Morocco(46)


 
Mpira uko ulaya.
 
Nashaangaa sana Switzerland na Netherlands
Wap wanampira mzur naona n Netherlands
Lkn cjui n kigezo gan kinawapandisha
Switzerland juu ya Netherlands
Acha kukariri Fifa wanaangalia current form sio historia, yaan timu imeshindwa kufuzu world cup afu awe top ten, angalia km kuna German hapo
 
We are in the light track
 
Tanzania wameachwa mbali sana na India. wakati india wana miaka 20 tu tokea wanze kucheza mpira wa miguu.
 
Tunalud kinyume nyume badala ya kusonga Mbele tumebaki wakupiga hatua moja Mbele hatua mbili nyuma!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…