Ufaulu kidato cha sita watia shaka wadau wa elimu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165

Dar es Salaam. Wadau wa elimu nchini wameonyesha kushtushwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kuonyesha kuwa asilimia 95.98 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo bila kuwapo na mikakati inayoonekana ya kuboresha kiwango cha ufaulu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau hao walisema pamoja na matokeo hayo kuonyesha ongezeko la ufaulu, wana wasiwasi iwapo matokeo yaliyoandikwa kwenye karatasi yanaakisi ufahamu wa wanafunzi.

Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo (Chadema) alisema hakuna mkakati wowote uliochukuliwa na Serikali kuhakikisha ufaulu unaongezeka, hivyo ni jambo la kushangaza kuona matokeo yanaonyesha wanafunzi wamefanya vizuri kiasi hicho.

"Hapo kinachooneka goli limepanuliwa ili magoli yaingie zaidi kwani kati ya mwaka jana na mwaka huu kitu gani kimefanyika. Ukaguzi wa walimu na wanafunzi haufanyiki, ufaulu unaongezekaje?" alihoji Susan.
Aliongeza kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kutaka kuwaridhisha wazazi ambao walikata tamaa kutokana na matokeo mabaya ya wanafunzi wao kwa miaka miwili iliyopita.

"Walimu wanajua kuwa hata wasipofundisha wanafunzi kuna mtu huko juu atawafaulisha tu," alisema.

Mkurugenzi wa shirika la Uwezo linalojihusisha na masuala ya elimu, Ziada Mgalla alisema wanafunzi waliofaulu wanapaswa kupongezwa iwapo asilimia 95.98 ya ufaulu inawakilisha ufahamu wao.

Alisema historia inaonyesha kuwa wapo baadhi ya wanafunzi ambao walifaulu kwa kiwango kikubwa lakini hawakuwa na uwezo wa kufafanua kile walichokiandika kwenye mitihani jambo linalotia shaka kuwa huenda matokeo ‘yalichezewa'.

Akizungumzia sababu za shule za umma kufanya vibaya, mkurugenzi huyo alisema kuwa Serikali ijiulize kwa nini walimu wanaofundisha shule hizo wanafunzi wao hufeli, lakini wakienda kufundisha shule za binafsi, wanafunzi wao hufaulu.

"Suala siyo tu kuwa na walimu, wawasikilize wanapolalamika vinginevyo itafika wakati mwanafunzi wa sayansi ataonekana amefaulu lakini akifika kwenye upasuaji akashindwa kufanya kazi taifa likatia aibu," alisema.

Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Boniventura Godfrey alisema wakati watu wanashangilia matokeo hayo yaliyotajwa kuwa ni mazuri yakilinganishwa na miaka iliyotangulia, wadau wa elimu wanapaswa kujiuliza kwa nini shule za umma zilizokuwa zikiongoza miaka ya nyuma zinazidi kufanya vibaya.

Alisema Serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwa hata mazingira ya shule hizo kwa sasa yameharibika ikilinganishwa na ilivyokuwa siku za nyuma ingawa zina idadi kubwa ya walimu.

Godfrey alisema matokeo hayo hayana uhusiano wowote na mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa kuwa haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kukawa na mafanikio ya kiwango hicho.

"Sijui matokeo haya ni mazuri kwa namna gani kwa sababu wala BRN (Matokeo Makubwa Sasa) haiwezi kuwa na mafanikio ya haraka namna hii.

Ninadhani suala la kuangalia hapa ni kwa nini shule za umma zimefelisha huku za binafsi zikiendelea kuongoza," alisema.

Chanzo: Mwananchi

 

Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya wavulana mchepuo wa Sayansi ya Iyunga ya Jijini Mbeya, wakiwa wamesomangana katika chumba kimoja wakati wa masomo yao jana asubuhi. Mkuu wa Shule hiyo France Mng'ong'o, alisema kuwa kidato kimoja kina wanafunzi zaidi ya 100 na kutokana na upungufu wa walimu wanalazimika kusongamana ndani ya chumba kimoja kwa lengo la kumsikiliza mwalimu wa somo husika. Picha na Godfrey Kahango
 
Kwani mumesahau nchi hii inaendeshwa kisanii!!

Tumeshasahau kuongeza div 5
 
Reactions: BAK
BRN mlifikiri watu walilala?

Bibie, elimu ina misingi yake ambayo ni muhimu sana kuipitia hatua baada ya hatua, sio kama barabara za Dk. Magufuli ambazo unashusha greda, linaanza kukwangua barabara na magari yanaanza kupita.
 
Reactions: BAK
Kwani mumesahau nchi hii inaendeshwa kisanii!!

Tumeshasahau kuongeza div 5
Kuna jambo ambalo ndilo tunatakiwa kuliogopa zaidi kwenye matokeo haya kuliko matokeo yenyewe! Nilijaribu hili kuliongea mahali lakini sidhani kama nilieleweka!!! In short, wengi wa wanaoonekana wamefaulu sitarajii kama watapata university admission. Hili likitokea, watu wanaweza kuridhika kuona kumbe hata mtu mwenye Div III, say ya Point 12, anakosa University Admission.

WEngi wetu, si ajabu, tukiona mtu kama huyo anapelekwa Ualimu, tunaweza kuona FINE, kumbe wengi wao, hata wale wenye Div III, bado passing yao haina sifa za kwenda Ualimu kama tutachukulia old grading system as a benchmark. Lakini ni wangapi tutalamika tukiona wenye Div III wengi wao wamepelekwa Ualimu?? Tutaona sawa tu kumbe si sawa unless iwe Diploma. My bet ni kwamba, hii grading system inakusudia sana kupata wanafunzi wengi zaidi wa kwenda kusoma Ualimu... na kweli watawapata sana... mbaya sana, wengi wetu hata wale tunaolalamikia matokeo haya, bado wataona ni sawa!!

c.c JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
Inaweza kuwa sawa wamefaulu kwa kuwa hadi div IV wao wanacount eti ni ufaulu
 
Kinachoendelea nchini Mkuu NasDaz kuhusu Elimu hakikubaliki hata kidogo hakuna chochote kilichofanyika ili kuboresha elimu yetu inakuwa ni ya kiwango cha juu hivyo wanafunzi wengi wa kidatu cha nne na cha sita waweze kufanya vizuri. Kinachoendelea sasa hivi ni ujunga na uhuni wa hali ya juu wa kushusha viwango vya ufaulu ili kuongeza asilimia ya wafaulu. Kuna kila haja ya Watanzania popote pale tulipo kukemea uhuni huu unaofanywa na hii Serikali ili zitafutwe njia za kweli na bora za kuboresha elimu nchini na badala ya hizi njia za kihuni na kisanii ambazo haziboreshi elimu hata kwa asilimia moja.

 
Last edited by a moderator:
Mwaka 2014 kule Brazil, imesemwa wingi wa mgoli WC ulitokana na mipira iliyotengenezwa na NASA kwa kwa vipimo wanavyojua wao. Tumepata magoli ya kutosha.FIFA haikuongeza upana au urefu wa magoli, ilichofanya ni kutafuta chanzo cha tatizo.

Kinachofanyika nchini mwetu kinasikitisha sana. Tunajua mfumo wetu wa elimu una matatizo.
Ni kuanzia Walimu wanavyopatikana, mafunzo wanayopewa, masilahi yao yanavyozingatiwa na vitendea kazi wanavyopewa.

Kwa mwaka mmoja tangu matokeo mabaya hatujaonyeshwa kwanini kulikuwa na matokeo mabovu, na mkakati gani uliopo kuondoa tatizo husika. Haiwezekani katika kipindi cha miezi 10 serikali iweze kutafuta suluhu ya tatizo pana na kubwa kama la elimu.

Tunakumbuka mwaka jana walichukuliwa vijana wa div 4 ili kujaza highschool.
Inawezekanaje kwa muda mfupi kiaisi hicho, bila kuambiwa tatizo na mikakati tumepata jawabu rahisi sana kama tunalosoma.

Enedapo tumeweza kufanya hivi katika sekta ya elimu, sidhani kama tungeshindwa ku-balance bajeti yetu kwa mwaka mmoja.
Ni miezi 10 ile ile ya 'kuinua kiwango'' cha ufaulu ingeweza kutumika ku-balance bajeti, na ndani ya miaka 5 kuondoa umasikini.

Inakuwaje tatizo la elimu lipate ufumbuzi wa haraka kiasi hicho huku tatizo la umeme likiendelea kwa miaka 8 ya serikali ile ile. Inawezakanaje tatizo la elimu lipate ufumbuzi haraka wakati tatizo la mishahara ya walimu likiwa ni sugu na lisilo na jawabu.

Hatukatai kuongezeka kwa ufaulu, lakini hili la kutoka 40% kwenda 95 lazima lina sababu.
Je, sababu za kuanzisha Div 5 zimeondoka, au nini matokeo ya kuanzisha Div 5? Mbona hatuambiwi kitaalamu.

Tunachokifanya ni kubumba wataalamu na wasomi wa siku zijazo. Kama alivyosema Naz, huko nyuma tulikuwa na mfumo wa kidato cha sita ambao ulihitaji mtu apate principle 2 na subsidiary moja kuingia chuo kikuu.
Hii ina maana kwa wakati ule mtu aliweza kupata E 2 na S akajiunga na kozi za chuo.

Wataalamu wengi na maprofesa waliopo walitumia mfumo huo. Hii haina maana kuwa na A nyingi za ulaini ni kuongeza ufahamu. Watu wanakumbuka Div 1 au 2 za wakati huo zilikuwa haswa, kila mtu anazikubali. Je, utitiri wa sasa una maana tunafanikiwa?

Hoja hapa ni kuwa kiwango cha ufaulu si tatizo, tatizo ni kama watahiniwa watafikia kiwango kile kwa weledi.

Hapa ni mambo ya kisiasa tu hakuna lolote la maana.
Kinachofanywa ni kukuza div na kupanua wigo wake ili div 3 ionejane bora kuliko 4 na 5.

Lakini, je, hiyo 3 ina maana yoyote?
Je, hiyo 3 ya 2014 inalingana na ipi ya 1980,1990? Je, kama 3 ya kupanua magoli itakuwa sawa na 0 ya 1990 tutakuwa tunajenga taifa la aina gani? Tunamdanganya nani na kwa faida ya nani?

Kama tunavyoona shule za kata zikipigiwa upatu na kuwa ngazi za kisiasa, kinachoendelea ni kuzipa div 1 na 2 ili mbele ya safari ijengwe hoja. Wakati wanafanya hivyo kwetu, wao wako bize kutafutia watoto wao shule South Africa, India na kwingineko.

Sisi tunaendelea kushangilia maafa!
 
Nguruvi3, BAK,
Mliyosema ni sahihi kabisa... lakini bado nasisitiza Watanzania tuende mbali zaidi ya hapa!! Tuende mbali zaidi ya hapa kwa kuona si tu matokeo ni mabaya bali ni mabaya kwa kiasi gani... tuende mabli si tu kwa kusema yamechakachuliwa, bali yamechakachuliwa kwa kiasi gani!! Tukishafahamu hili, hata wahusika tunaweza kuwabana kwa hoja!! Mathalani, tuchukulie suala la Division V. Kauli ya Waziri Kawambwa, and in fact ndivyo ukweli ulivyo, ukishakuwa na Division V huendi popote... kwahiyo hata Wizara ukiwabana kwa kufuta Zero, bado watakuambia hata hiyo Div 5 is almost zero... hakuna kilichobadilika coz' mwenye Div V haendi popote kama ilivyokuwa kwa mwenye ZERO!!! Division V or FAILED is just a name what matters is just content and its application.

Ninachomaanisha ni nini?? Assume kijana aliyemaliza Form VI na kuwa na C flat! Baada ya hapo watu tukajikita kwenye matokeo kuchakachuliwa bila kutafuta yamechakachuliwa kwa kiasi gani. Sasa basi, huyo mwenye C flat tutaona nae ni matokeo ya uchakachuzi. Huyo, assume amechaguliwa kusoma Engineering tutazidi kusimamia hoja yetu ya uchakachuzi na kuwa na nguvi kweli kweli!!! But what if ikaonekana huyo mwenye C flat amekosa kuchaguliwa university lakini amechaguliwa Ualimu, Diploma Level. Endapo hatutajikita kwenye ni namna gani haya matokeo yamechakachuliwa kwa kiasi gani, watu tunaweza kuridhika kwamba, kwavile wenye C flat hawakupata university admission basi effect yake ni ndogo... kwavile huyo mwenye C Flat stahiki yake ni Ualimu... hivi ndivyo wakina Kawambwa watakavyojitetea, sawa na wanavyojitetea kwenye suala la Div. 5!

Naweka angalizo hili kwavile watu tunaweza kuishia kuangalia, je miongoni mwa hao 95%, ni wangapi wamepata university admission bila kuangalia other sensitive areas of education level kama vile middle Teachers' and Health Colleges. Kwamba, sawa assume huyo mwenye C Flat amekosa university admission, BRILLIANT, lakini amechaguliwa kusoma Diploma in Pharmacy... je, pamoja na C zako hizo, assuming pasingekuwa na uchakachuzi, je bado alistahili kusoma hiyo Diploma?

Au twende mbali zaidi kwa kuangalia barua ya Wizara ya mwaka jana. Sehemu ya barua inasema: "Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumohuu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa
upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E
= 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39." Kisha inaendelea: "Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia...." Kisha wanaendelea, "Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini: A 75 - 100, B+ 60 - 74, B 50- 59, C 40 - 49, D 30 - 39, E 20 - 29, F 0 - 19. Sasa, tu-assume kwamba grading system iliyotumika ina-comply hiyo barua ya Wizara... hii maana yake nini, huyo mwenye C, 40-49 mwaka 2014(look RED), ingekuwa ni mwaka 2012 angedondokea ama kwenye E= 45 – 54; au S = 40 – 44 and net outcome becoming hizo C Flat si tu kwamba Not C Flat, but not even D Flat but either E Flat or S Flat or the chemistry of E and S!!!

Sasa ikiwa mwenye C Flat can lie somewhere either in E or S, what about mwenye D Flat? Jibu la hili, utalipata hata kwenye matokeo yenyewe. Nimejaribu kuangalia matokeo ya shule kadhaa... Division IV, hazijaandikiwa Point!!!! Be reminded, ukiwa na D Flat, unakuwa na Division IV lakini hamna point!! Tafsiri yake ni nini, D ina-range between 30-39 (2014) lakini 30-39 in 2012 inadondokea kwenye F 0-39!!! Which means, our today's D Flat, could be F flat kama tutatumia system ya 2012. Sasa je, huyu mwenye D Flat hawezi kupelekwa Ualimu huyu wakati kimsingi ana F Flat?? This's important to know coz' before 2013, mwenye D flat angeweza kupata university admission. Sasa, akina Kawambwa wanaweza kutumia lugha ile ile kwamba, huyo mwenye D flat zamani alikuwa anaenda chuo kikuu lakini kwa mfumo wa sasa, hawezi kuchaguliwa chuo kikuu... maskini ya mungu kumbe amechaguliwa Ualimu wakati ana F flat!!!
 
Last edited by a moderator:
Another interesting finding kwenye haya matokeo! Shule inayoongoza Tanzania mzima, Igowore Secondary School, haina A hata moja. Mkali kabisa ana B+ Flat, tena only one student. According to bara ya Wizara, B+= 60-74... kwa miaka ya nyuma, 60-74=C... kwahiyo, shule inayoongoza, mkali wa darasa ingekuwa ni old grading system, angekuwa na I, point 9 (one ya mwisho) na wengine wote ni ama II or III!! Lakini shule hiyo hiyo hapa ambayo mwaka huu ndio kinara, mwaka jana walikuwa na Div I moja tu, tena ya Point 9 (reflecting mawazo yangu hayo juu... kwamba, hata matokeo ya mwaka huu, ingekuwa ni old system, kuna I moja tu tena ya point 9, like 2013!!!)

Didn't I say hawa wa mwaka huu, mkali kabisa ana C flat (basing on old system), nor B or A? Hata mwaka 2013, shule mzima hawakuwa na B wala A... what a coincidence!! Anyway, it doesn't prove anything but interesting kuona shule ambayo darasa zima wana II na III with only one Div I, ndiyo inaongoza Tanzania mzima!!!
 
ifike wakati serikal isikimbie ukwel na kuanza kutafuta njia mbadala katika suala la elimu. Tatizo la elimu nchini litaisha endapo WALIMU wataboreshewa maslai yao tu. haiwezekan mtu ambaye hakuangaika kutafuta elimu just form four lakin mshahara wake ni mkubwa tena ana leshen kila katikati ya mwezi maduka yao ni duty free mwalimu Wa TGTS C analipwa 382 000/= hiyo ni take home tena huyo ana dioloma. sasa sijui yule Wa ngazi ya cheti ambao ni primary teachers hali ikoje.
 
ccm imeamua kuua elimu yetu na sisi wananchi tumeamua kulalamika bila kuchukua hatua je tutafika?
 
Reactions: BAK
Wakifeli majanga, wakifaulishwa matatizo...

kuanzia 2008 kurudi miaka ya nyuma hapakuwa na kelele za matokeo hayo makelele yameanza 2012 pale necta walipoanza kutumia mifumo mipya ya upangaji wa madaraja wangeacha kama mwanzo na kubadilisha silabasi kila wakati pia nalo tatizo mkuu
 
Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??
Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!
Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!!"
 
Nafikiri wizara ya elimu ilikaa chini na TCU wakabuni mkakati madhubuti wa kuziba pengo kubwa vyuoni lililoachwa kutokana na wanafunzi wengi wa kidato cha nne mwaka juzi kufeli vibaya.
 

MWAKA 2013: A = 80 – 100; B = 75 - 79;
C = 65 – 74; D = 55 – 64; E= 45 – 54; S =
40 – 44 na F =0 – 39.
Hivyo vilikuwa viwango vya ufaulu 2013
linganisha na vya sasa.
 
Mkuu umewashughulikia!! Watu mnajua kuchimbua kwa undani, sisi wengine tumepita tu baada ya kuambiwa Igowore imeongoza tukasema haya bwana!! Kumbe ni madudu matupu! Kwa kweli siasa inatuharibia mambo, sasa hapo raia tumedanganywa kwamba matokeo yako vizuri mno kumbe upuuzi mtupu! Anyway, ndo BRN ya Kikw.ete. hiyo! Kwa upumbavu wetu 2015 tunatoa tena kama mataahira vile. Hivi ni nani anategemea mabadiliko kwa akili hii ya kina Simiyu Yetu, Ifweero, Mamndenyi, Kilambalambila, Mmaranguoroginal, CHOONI, Maguzumasese, FaizaFuska, Masopakyindi, Malaria Sugu (sijui alifia wapi) na wengine wengi Wa aina hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…